Zinazobamba

MSAMA PROMOTIONS YAWATAMBULISHA BAADHI YA WAIMBAJI WA NYIMBO ZA INJILI TAMASHA LA PASAKA

 


Na Mussa Augustine.

Kampuni ya Msama Promotion ambayo imeandaa tamasha kubwa la Pasaka  imetaja baadhi ya Waimbaji wa Nyimbo za Injili  ambao wamethibitisha kuwepo katika tamasha hilo litakalofanyika April .9. 2023, katika Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es salaam.

Akizungumza na Waandishi wa habari Februari 24.2023 jijini Dar es salaam, Mkurugenzi wa kampumi hiyo Alex Msama amesema kwamba tamasha la awamu hii litakua la aina yake kwani waimbaji nguli wa nyimbo za injili kutoka ndani na nje ya Tanzania wanatarajiwa kushiriki.

Mkurugenzi huyo pia amesema kwamba Tamasha hilo linaenda samabamba na sherehe za miaka miwili ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan tangu aingie madarakani baada ya mtangulizi wake Hayati Dkt Jonh Magufuli kufariki dunia.

“Siku ya Tamasha la Pasaka tutaliombea  Taifa letu na Viongozi akiwemo Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa na nzuri anayoifanya ya kuwatumikia Watanzania na  kuliletea Taifa letu Maendeleo,tumekuwa tukishuhudia majanga mbalimbali yanajitokeza kwa nchi zingine hivyo kupitia tamasha hili tutafanya maombi ya kulinusuru Taifa letu na majanga mbalimbali kama vile Vita,Ukame , Njaa na Mafuriko”amesema

Msama amesema Kwamba Tayari Baadhi ya Waimbaji Nguli wa Nyimbo za Injili kutoka Hapa Nchini na Nje ya Nchi wamethibitisha kushiriki katika Tamasha hilo lianalotarajiwa kuwa na mambo mengi mbalimbali yatakayofanyika huku akiwaomba watanzania kujitokeza kwa wingi kushuhudia na kuimba kwa pamoja kwa ajili ya kumsifu Mungu.

“Waimbaji waliothibitisha kushiriki Tamasha hili  ni Tumaini Akilimari kutoka Kenya,Joshua Ngoma kutoka Rwanda,Upendo Nkone  ,Ambwene Mwasongwe  hawa nikutoka Tanzania,pamoja na Mwimbaji Masi Masilia kutoka nchini Kongo ambaye anakuja kwa mara ya kwanza  hapa nchini hivyo Watanzania  wajitokeze kwa wingi kushuhudia tamasha hili” amesema  kwa bashasha kubwa.

Nkuongeza kuwa “bado tunaendelea kufanya mazungumzo na waimbaji wengine kutoka Mataifa mbalimbali ikiwemo Afrika Kusini,Uingereza na Marekani ili washiriki katika Tamasha hili ,hivyo wale watakaokubali kushiriki tutaendelea kuwafahamisha Watanzania,lakini kuna baadhi ya kwaya zimekubali kushirikiana nasi  ikiwemo Zabron Singers.


Hakuna maoni