Zinazobamba

Baraza la Madiwani Kinondoni Laiangukia Serikali Kuhusu Biashara ya Ngono

 

Diwani wa Kata ya Mzimuni Manispaa ya Kinondoni Manfred Lyoto 

Na Mussa Augustine

Baraza la Madiwani katika  Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni imeiomba serikali kupitia Wizara ya Maendeleo ya Jamii,Wanawake na Makundi Maalum kuingilia kati kukithiri kwa biashara ya ngono na ujenzi wa madanguro katika Wilaya hiyo.

Baraza hilo pia limeadhimia kumuita Waziri Dkt Dorothy Gwajima anayeshughulikia masuala ya Maendeleo ya Jamii,Wanawake na , Makundi maalumu kuweza kufika na kujionea hali halisi ya kukithiri kwa bishara hiyo ili aweze kusaidia kuchukua hatua za kuthibiti hali hiyo.

Akizungumza wakati wa kikato cha kawaida cha baraza hilo Februari 22.2023 Meya wa Manispaa ya Kinondoni Songoro Mnyonge amesema kwamba hali ya biashara haramu ya ngono ni mbaya zaida katika wilaya hiyo.

Aidha amesema kuwa wanaiomba Wizara ya Maendeleo ya Jamii,Wanawake na Makundi Maalumu iache kujikita pekee katika eneo moja la ukatili dhidi ya mtoto badala yake iangalie na athari zinazojitokeza kutokana na  makundi mengine.

Amesema kuwa Wilayani humo nyumba zimegeuzwa kuwa Madanguro kutokana na hivi sasa nyumba za kupangisha zimebadilishwa matumizi nakuwa madanguro  ambapo wamiliki wanaamini kufanya hivyo wanaingiza fedha nyingi kuliko kupangisha wapangaji wa kawaida.

“Katika kata ya Mwananyamala madanguro yamefikia 150 wamiliki wanakata nyumba katika vyumba vidogo vidogo vyenye mlango mbele na nyuma”.

Nakuongeza kuwa “Mteja anaingilia mlango wa mbele anatokea mlango wa nyuma kumpisha mwingine aingie”alisema

Aliendelea kufafanua kuwa biashara hiyo pia imeshika kasi wilayani humo ambapo katika Hoteli na Nyumba za kukanda mwili yaani Massage zimekuwa kichocheo cha kufanya ngono zembe.

“Masaji zingine za mwili mzima ,wanaofanya masaji wanateremka hadi maeneo ya mwili ambayo hayastahili ,huu ni ushawishi wa ngono zembe”amesema Meya Mnyonge.

Aidha amesisitiza kuwa Madanguro hayo ni chanzo kikubwa cha athari ya kimaadili kwa watoto “Mambo yanayofanywa na watoto wadogo sasa hivi inawezekana kuna watu wazima hawawezi kuyafanya ,watoto mwanajua mambo makubwa na mazito ambayo mtu mzima hakuwahi kuyapitia”alisema

Diwani wa Kata ya Mzimuni Manispaa ya Kinondoni Manfred Lyoto

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi Kando ya kikao cha Baraza hilo Madiwani ,Diwani wa Kata ya Mzimuni Manispaa ya Kinondoni Manfred Lyoto amesema kwamba hali hiyo niyakusikitisha kwani inafanywa na watu ambao wengi wao wana umri mdogo.

“Halmashauri yetu imeonekana kwenda tofauti na na maadili  yetu ya Kitanzania na hata kiafrika,na hili suala linatakiwa kuratibiwa vizuri ili kuchukua hatua stahiki kwani bila kufanya hivyo biashara hii ya ngono na kujengwa Madanguro haitakomeshwa.

“Tumejaribu kufanya utafiti hadi tukafikia kipindi tukawabaini baadhi yao wasio na kazi za kuwaingizia kipato cha halili,lakini tulipowataka kuwaingiza katika mpango wa kuwapatia fursa yakufanya kazi za maana hawakujitokeza,walijitokeza watu watatu kati ya ishirini wengine waliendelea kufanya biashara za ngono,kwahiyo ni suala ambalo kama nchi lazima tujaribu kuliangalia manake sio sababu ya ugumu wa maisha ndo unachangia kufanya hivyo”alisema Diwani Lyoto

Hakuna maoni