Zinazobamba

HAKIELIMU YATOA TAMKO JUU YA ADHABU ILIYOPELEKEA KIFO CHA MWANAFUNZI MWANZA

Mkurugenzi Mtendaji Dkt Jonh Kalage (mwenyemkoti katikati) akizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani wakati akitoa tamko la Taasisi hiyo kufuatia adhabu iliyopelekea kifo cha mwanafunzi Mkoani Mwanza.


Na Mussa Augustine 

Taasisi ya Hakielimu imeiomba Serikali kurejea upya  mapendekezo yanayotolewa na wadau wa elimu  kuhusu matumizi ya lugha ya kiswahili kama lugha ya kufundishia ngazi ya sekondari.

Rai hiyo imetolewa leo na taasisi hiyo kupitia Mkurugenzi Mtendaji Dkt Jonh Kalage wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam kufuatia tukio la adhabu iliyopelekea kifo cha mwanafunzi Gloria Faustine wa kidato cha kwanza katika shule ya sekondari Mwinuko Manispaa ya Ilemela Mkoani Mwanza.

Dkt Kalage amesema kwamba Watoto wanaotoka shule za msingi na hasa za umma kuingia kidato cha  kwanza wanakua hawajawa tayari kuweza kutumia lugha ya kiingereza katika kuzungumza na kujifunzia hivyo kutumia kiswahili kama lugha ya kufundishia sekondari itatoa fursa kwa watoto kujifunza kwa ufasaha na kufundishwa vema kingereza na lugha nyingine kama lugha za kigeni.

Aidha amesema kwamba taasisi hiyo pia imependekeza dhana ya adhabu chanya kupewa mkazo katika mafunzo darasani na kazini kwa walimu ili kuwasaidia kuepukana na matumizi ya adhabu za kikatili akitolea mfano wakati wa mafunzo kwa vitendo kwa walimu utoaji wa adhabu unaweza kuwa moja ya eneo la tathmini.

" Hakielimu hatupingi kutumia lugha ya kingereza sekondari, bali tunapinga lugha hii ya kingereza kutumika kama lugha ya kufundishia, pia tunaendelea kusisitiza matumizi ya adhabu chanya na vichocheo chanya katika kuimarisha nidhamu na kujifunza,amesema Dkt Kalage.


Baadhi ya Waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari wakimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Hakielimu Dkt Jonh Kalage(hayupo pichani).

Kwa upande wake Mshauri  Mwelekezi wa Hakielimu Wilberforce Meena amesema.kwamba taasisi hiyo haipingi matumizi ya lugha ya kingereza katika shule za sekondari bali lugha hiyo iwe kama lugha ya kigeni kwa ajili ya mawasiliano huku  lugha ya kiswahili itumike kama lugha ya kufundishia.



Hakuna maoni