Zinazobamba

WAZIRI ULEGA KUWA MGENI RASMI KWENYE SHINDANO LA KUHIFADHI QURAN TUKUFU

                                         Maulid Kitenge 

Na Mussa Augustine

Waziri wa Mifugo na Uvuvu Abdallah Ulega anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye fainali za Mashindano ya kuhifadhi Qur'an Takatifu yanayofanyika kitaifa Kwa kukutanisha madrasa zote nchi nzima

Hayo yamesemwa Machi 23 ,2023 Jijini Dar es Salaam na Maulidi Kitenge ambaye ni Mlezi wa Madrasati Nnijuum kupitia Kituo Cha Tanzania Annujuum Islamic Centre ambayo imeandaa Mashindano hayo ikiwa lengo ni kuwafanya watoto waweze kuhifadhi Qur'an Takatifu.

Maulidi Kitenge ambaye pia ni Mtangazaji wa redio ya  E.fm, amesema kwamba fainali hizo zitafanyika Jumapili   ya tarehe 26 Mwezi Machi 26, 2023 katika Ukumbi wa DYCC YEMEN uliopo Chang'ombe Wilayani Temeke,ambapo wageni mashuhuli watakuwepo katika Mashindano hayo.

Aidha amesema kuwa kuhifadhi Qur'an Takatifu Kwa watoto wadogo inasaidia Kwa kiasi kikubwa kujifunza tabia njema na maadili mazuri ya kidini wakiwa katika umri mdogo.

"Tunatarajia Mgeni rasmi atakua Abdallah Ulega Waziri wa Mifugo na uvuvi kwani amewahi kujifunza madrasa akiwa mdogo,hivyo zitakuwa fainali za aina yake kwasabubu pia kutakuwepo na wageni mbalimbali mashuhuri," amesema Kitenge.

Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu Madrasati Nnijuum Mustafa Ally amebainisha kwamba lengo la kuzikutanisha madrasa zote nchini kwenye shindano hilo ni kubadilisha muonekano wa tafsiri za madrasa kuwa zinafundisha mambo yasiyofaa Kwa watoto,nakuifanya jamii itambue kuwa madrasa zinafundisha maadili mazuri Kwa watoto.

"Ndugu zangu waandishi wa habari fainali hizo zimegawanyika katika makundi manne ambapo kundi la kwanza nila watoto wanaohifadhi juzuu 3, kundi la pili Juzuu 15,kundi la tatu Juzuu 20 na Kundi la nne Juzuu 30 " amesema Naibu  Katibu Mkuu huyo wa Madrasati.

Nakuongeza kwamba" Washindi wa Kila kundi watapata zawadi ambapo hatutazitaja hapa itakua ni surprise siku hiyo hivyo naomba watu Wajitokeze Kwa wingi kushuhudia Mashindano hayo ambayo yanafanyika Kwa mara ya kwanza Kwa kushindanisha madrasa zote nchi nzima na tunatarajia yatakuwa endelevu.

Nae Irene Kilenga maarufu kama Baby Mama ambaye pia ni Mlezi wa Madrasati Nnijuum amesema kuwa katika kipindi hiki Cha mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani Mashindano hayo yatasaidia kutekeleza Ibada ya Funga Kwa Waumini wa Kiislam, hivyo amewaomba wazazi na walezi wajitokeze kushuhudia namna watoto wao wanavyoshindana kuhifadhi Qur'an Takatifu.

Hakuna maoni