Na Mussa Augustine
Chama Cha Wafanyabiashara wenye
Viwanda na Kilimo (TCCIA) imeiomba serikali kupitia Mamlaka ya Mapato Nchini (
TRA) kuweka utamaduni wa kukutana na wafanyabiashara kujadili namna ya kuweka
mifuno mizuri ya ukusanyaji wa kodi stahiki hali itakayosaidia wafanyabiashara
hao kulipa kodi kwa hiari nakwa wakati.
Rai hiyo imetolewa leo na Mkurugenzi
Mkuu wa TCCIA Nebart Mwapwele wakati wa majadiliano ya mradi wa Husisha kwa
maendeleo Endelevu unaotekelezwa na TCCIA kwa kushirikiana na TRIAS, ambapo
majadiliano hayo yamelenga kuondoa changamoto zinazowakabili wafanyabiashara
wakati wa kulipa kodi.
Aidha amesema kuwepo kwa majadiliano
ya mara kwa mara kati ya TRA na wafanyabiashara inasaidia kutoa elimu ya
kuboresha mifumo ya upimaji kodi kwa hiari nakuondoa njia ya matumizi ya nguvu.
Mjadala huo umewakutanisha wadau
mbalimbali kutoka makampuni 50 ya wafanyabiashara,sekta za huduma kama vile
Watunga sera za kodi,wasimamizi wa kodi,wadau wa maendeleo ,wataalamu wa kodi ,
Wanataaluma , Mashirika ya utafiti, wadau kutoka Wizara ya fedha na mipango ili
kujadili kwa pamoja changamoto zinazowakabili wafanyabiashara nakushindwa
kulipa kodi kwa wakati.
"Mjadala huu unahisi masuala ya
kodi,hatuna washiriki wa sekta mbalimbali ikiwemo TRA na taasisi ambazo
zinawasimamia wafanyabaishara ,lengo ni kumpa mfanyabiashara elimu kuhusu
masuala ya kodi ili alipe kodi stahiki na kwa hiari" alisema
Naye Makamu Rais Biashara TCCIA Dkt
Kulwa Meshack amesema kwamba wamekuwa wakihamasisha wanachama wa TCCIA walipe
kodi kama wajibu wao kwa mujibu wa sheria ili kuondoa misuguano kati ya TRA na
Wafanyabiashara hao.
Amesema kwamba TCCIA imekua
ikishirikiana Vizuri na TRA kupitia kitengo cha huduma kwa mlipa kodi
kuelimisha wanachama kuhusu elimu ya kodi nakuondoa mifumo mibovu ya ulipaji
kodi inayowaumiza wanachama.
" Hakuna sababu yakusema
tumekadiria vibaya na TRA wametusikia hivyo malalamiko ya kutozwa kodi isiyo
stahiki yatakwisha kwasababu tunaendelea kujadiliana na TRA kuangalia mifumo
yote mibovu ya kulipia kodi nakuweza mifumo mizuri " amesema
Dkt Meshack
Kwa upande wake Meneja Elimu kwa
Mlipa Kodi kutoka TRA JUlius Mjenga amesema wamesikiliza maoni na mapendekezo
ya wadau hao nakwamba TRA inaendelea kuyafanyia kazi maeneo ambayo bado
yanaleta ukakasi wa kulipa kodi kwa wafanyabiashara hao.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni