Zinazobamba

TANESCO Yafanya Jitihada za Kupunguza Makali ya Mgao wa Umeme

 


Mkurugenzi Mkuu wa TANESCO Maharage Chande

Na Mussa Augustine.

Shirika  la Ugavi wa Umeme Nchini (TANESCO),limesema wakati huu wa  kipindi kifupi limefanya jitihada za kupunguza makali ya mgao wa umeme kwa kufanya marekebisho ya mtambo mmoja ubungo na kusaidia kuingiza megawati 35 katika gridi ya Taifa  na Mtambo mmoja wa kituo cha kinyerezi namba 2 Umekamilika na kuzalisha megawati 215 za umeme.

Pia,TANESCO  imesema imeshakamilisha matengenezo ya mtambo mmoja wa kituo cha kidatu na kuanza kuzalisha megawati 50 za umeme katika gridi ya Taifa kuanzia novembe 24 mwaka huu.

Hayo yameelezwa  leo Jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mkuu wa TANESCO,Maharage Chande,wakati akizungumza na waandishi wa habari wakati akitoa taarifa kuhusu Jitihada  zinazofanywa na shirika hilo kukabiliana na upungufu wa uzalishaji wa umeme uliojitokeza kutokana na kuwepo kwa ukame.

Chande amesema kutokana na matengenezo hayo kukamilika imepelekea kupungua kwa wastani wa kati ya megawati 300 hadi 350 wiki iliyopita hadi kufikia megawati 215 za umeme wiki hii

Aidha,Chande,amesema mvua zilizonyesha maeneo mbalimbali nchini hazaweza kujaza kwenye mabwawa ya kuzalisha umeme ya Pangani na Kihansi na kupelekea kuendelea kuwepo kwa upungufu wa umeme kwenye gridi ya taifa.

Hata hivyo,Chande,amesema iwapo mvua zitaendelea kunyesha katika mabwawa yote ya kufua umeme na matengenezo yaliobaki kukamilika kama yalivyopangwa  yatasaidia kumalizika mgao wa umeme.

 

Hakuna maoni