Tamasha Kubwa la Uimbaji na Miujiza Limeanza leo Jijini Dar es salaam
Na Mussa
Augustine.
Mwinjilisti
wa Kimatiafa Kutoka Nchini CANADA Dkt Piter Youngren amewasili nchini
Tanzania kwa mara nyingine kwa ajili ya tamasha kubwa la siku tatu la
uimbaji na Miujiza litakalofanyika katika kanisa la BCIC Mbezi Beach Jijini Dar
es salaam linalongozwa na Askofu Mkuu Sylvester Gamanywa.
Akizungumza
mara baada ya kupokelewa Kanisani hapo Dkt Youngren amesema kuwa maombezi hayo
yatalenga kuombea maisha ya Watanzania waliokumbwa na matatizo mbalimbali
pamoja na kuliombea Taifa kutokana na kukumbwa na majanga mbalimbali
yakiuchumi, Kisiasa na kijamii
Dkt
Youngren amesema kwamba maombi hayo ya siku tatu ambayo yameanza leo Desemba 2
hadi 4 yatasaidia kuwaondolea changamoto mbalimbali Watanzania wenye
changamoto mbalimbali ikiwemo magonjwa,ukosefu wa Ajira,Ukraine pamoja na
migogoro ya ndoa,inayowafanya wakate tamaa katika maisha yao.
"Kila
wakati wa majanga ni fursa, Ulimwengu unakabiliwa na majanga , Uchumi
kuporomoka haya yanatufanya sisi viongozi wa dini tufanye mambo mazuri
zaidi katika maombezi yetu hivyo tunachohitaji ni ufahamu mpya katika wakati
huu changamoto kwani ni mkakati za fursa " alisema Dkt Youngren.
Kwa Upande
wake Askofu Mkuu wa Kanisa la BCIC Askofu Silvester Gamanywa amesema
kwamba wanatarajia mabadiliko makubwa yakiroho na kiuchumi kupitia tamasha hilo
la uimbaji na miujiza hivyo ameiomba jamii kujitokeza kwa wingi kushiriki
katika tamasha hilo.
"Maombi
haya nikwa ajili ya kuombea Jamii na Taifa kwa ujumla , tunatarajia matokeo
makubwa, nawaomba watu wenye matatizo mbalimbali waje wapate huduma ya maombezi
katika tamasha hili la historia" alisisitiza Askofu Gamanywa.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni