Zinazobamba

Ripoti Ya Awali Kuhusu Ajali ya Ndege ya Precision Air Yatolewa Rasmi na Serikali



Na Mussa Augustine.

Waziri  wa Ujenzi na Uchukuzi Profesa Makame Mbarawa amesema mlango wa ndege ya shirika la ndege la Precision Air iliyopata ajali ziwa Victoria ikijaribu kutua Bukoba ulifunguliwa na mhudumu akisaidiana na abiria.

Akitoa ripoti ya uchunguzi wa ajali hiyo Novemba 24 jijini Dar es salaam, Waziri Mbarawa amesema wavuvi walifika katika eneo la ajali hiyo mwendo wa dakika tano tangu itokee na kwamba jitihada za wao kujaribu kufungua mlango ziliwaongezea ari mhudumu na abiria kufungua mlango.

Mbarawa amesema hali ya hewa ilibadilika ghafla na boti ya uokozi ilichelewa kwa kuwa ilikuwa doria. Ripoti hiyo kwa mujibu wa Waziri anayehusika na uchukuzi haikutaja majina.

“Ni kweli mlango ulifunguliwa na mhudumu wa ndege kwa msaada wa abiria, hata hivyo kama ripoti ya uchunguzi inavyosema wananchi waliokuwa wanafanya shughuli za uvuvi walifika eneo la ajali dakika 5 baada ya ndege kuanguka,” amesema.

Aidha amesema kwamba kuna baadhi ya masuala yamejitokeza katika ripoti ya awali la kwanza hali ya hewa ambapo ripoti inasema kuwa iliripotiwa kuwa hali ni nzuri mpaka saa 2 asubuhi ambapo ilibadilika ghafla na mvua kuanza kunyesha ikiambatana na radi,nakubainisha kuwa ndege hiyo iliingia anga ya Bukoba saa 2:45 na kukuta hali ya hewa imebadilika Amesema Profesa Mbarawa.


Aidha amesema kwamba ngege ilizunguka takribani dakika 20 ikitarajia uwezekano wa hali ya hewa kubadilika baadae rubani aliamua kutafuta njia ya kuruka kutokana na maelezo ya abiria walionusurika ,njia ya ndege ilikuwa inaonekana.

Hata hivyo pamoja na mambo mengine Profesa Mbarawa ameitaka jamii kuacha kusikiliza taarifa za upotoshaji zinazotolewa na watu mbalimbali ikiwemo wanasiasa na badala yake wafuate taarifa zinazotolewa na serikali kupitia Wizara  yake  ya Ujenzi na Uchukuzi.

Hakuna maoni