Zinazobamba

Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Yatoa Elimu Matumizi ya Mtandao.

Na Mussa Augustine.

Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari imetoa elimu ya matumizi sahihi ya mitandao ya kijamii kwa baadhi ya wanafunzi wa shule ya sekondari ya Wasichana Jangwani jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na waandishi wa  habari shuleni hapo Mkurugenzi wa Masuala ya Mtandaoni kutoka Wizara hiyo Mhandisi Steven Wangwe amesema kuwa wanatoa elimu hiyo ikiwa ni utekelezaji wa kampeni ya mwezi wa kutoa elimu kuhusu matumizi sahihi ya mitandao ya kijamii kama vile Twitter 'Instagram  na Facebook.

Mhandisi Wangwe amesema kuwa licha ya kutoa elimu shule ya sekondari ya Wasichana Jangwani ,Wizara hiyo intarajia kutoa elimu hiyo maeneo mbalimbali nchini ili kuwezesha wanafunzi na jamii kwa jumla kuacha kutumia vibaya mitandao hiyo kwa kuchapisha jumbe zisizofaa pamoja na kuposti picha ambazo hazina maadili.

"Wizara ya habari,Mawasiliano na Teknolojia ya habari tunatoa elimu kuhusu matumizi sahihi ya mitandao ya kijamii,mwezi mmoja tunautumia kutoa elimu katika maeneo mbalimbali ili kusaidia kuzingatia maadili kwenye mitandao"amesema Mhandisi Wangwe.

Kwa upande wake mwalimu wa shule ya sekondari ya Wasichana Jangwani Salum Kilipamwambu amesema kuwa elimu hiyo inasaidia wanafunzi kujitambua nakuwezesha kujikita kwenye masomo nakuachana na tabia ya kuposti mambo yasiyofaa mtandaoni.

Aidha amesema kuwa Wizara hiyo imefanya jambo jema kutoa elimu shuleni hapo kwani atua hiyo itawafanya wanafunzi kutumia vizuri mitandao ya kijamii, nakusaidia wanafunzi kutumia mitandao hiyo kwa manufaa yao ya masomo.

"Somo la teknolojia ya habari na Mwasailiano(TEHAMA) shuleni linafundishwa lakini halipewi kipaumbele katika ufundishwaji ,hivyo tunaiomba serikali itilie mkazo somo hili muhimu kwa wanafunzi ili wajue mapema matumizi sahihi ya mtandao"amesema Mwalimu Kilipamwambu.
Kwa upande wao baadhi ya wanafunzi waliyopewa elimu juu ya matumizi usahihi ya mitandao akiwemo Anna Ngowi ambaye anasoma kidato cha 6 shuleni hapo amesema hatua ya Wizara ya habari kutoa elimu hiyo ni yakuungwa mkono kwani imewapa elimu nzuri juu ya jinsi gani wataepuka matumizi mabaya ya mitandao ya kijamii.

"Kwa sisi wanafunzi tunashukuru kwa kupewa elimu hii,na tumejifunza ni vitu gani vya kuposti na visivyo vya kupost mitandaoni ili visitudhalilishe na kupelekea kuwepo kwa vitendo vya unyanyasaji wa kimtandao (cyber bullying)hivyo nawaomba vijana wenzangu hasa wanafunzi watumie vyema mitandao"amesema Neema Matilda ambaye ni wanafunzi wa kidato cha 5 shuleni hapo.

Hakuna maoni