Zinazobamba

Islamic Education Panel yatangaza Matokeo ya mtihani wa Dini 2022

Mjumbe wa jopo la wataalam wa elimu ya kiislamu IEP Sheikh Mussa Yusuph Kundecha ametangaza matokeo ya mtihani wa darasa la saba wa elimu ya dini ya kiislamu uliofanyika septemba 14,2022 na kusema kuwa jumla ya shule 3710 katika mikoa 25 na halmashauri 151 zilishiriki kufanya mtihani huo.

Akizungumzia na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam wakati wa kutangaza matokeo hayo,Sheikh Kundecha amesema kuwa jumla ya watahiniwa waliosajiliwa walikuwa 163,143 na waliofanya mtihani ni 142,522 sawa na asilimia 87.36 

Aidha ameendelea kusema kuwa  idadi ya watahimiwa ambao hawakufanya mtihani huo kutokana na sababu mbalimbali ni 20621.

Amesema idadi ya watahiniwa waliofaulu kwa kupataa daraja A hadi C ni 95,166 sawa na asilimia 66.77 ya watahiniwa wote 142522.

Aidha amesema idadi ya watahiniwa waliopata madaraja ya D na E ni 47,356 sawa na asilimia 33.23 ya watahiniwa wote waliofanya mtihani.

"ndugu wanahabari idadi ya watahiniwa na madaraja yao ni kama ifuatavyo waliopata daraja la kwanza (A) ni wanafunzi 3,567,daraja la pili (B) ni wanafunzi 22,587,daraja la tatu (C)ni 69,012,daraja la nne (D)45,781 huku.daraja la mwisho (E) ikiwa ni 15,575"amesema mjumbe huyo wa IEP 

Akizitaja shule 10 bora katika la shule zenye watahiniwa 20 na kuendelea, Sheikh Kundecha amezitaja kuwa ni *Mumtaz (Mwanza),Istiqaama(Tabora),Rahma (Dodoma),Algebra Islamic(Dar es salaam),Dumila(Morogoro)Islamiya(Mwanza)Hedaru (Kilimanjaro),Daarul Arqaam(Dar es salaam),Mbagala Islami(Dar es salaam pamoja na Maarifa Islamic (Dar es salaam

Hata hivyo amesema kuwa shule 10 za mwisho zilizopata ufaulu mdogo kabisa ni pamoja na shule za msingi  Kilimani (Ilala),Mwasenga(Kigoma Ujiji),Umoja (Tabora),Bugoyi (Shinyanga),Mvuti(Dar es salaam)Kasamwa(Geita),Muzdalifa Islamic(Lindi),Mawala (Kilimanjaro)Sipungu (Tabora)pamoja na Izumangabo (Geita)

Katika hatua nyingine Sheikh Kundecha ambaye pia ni  mkuu wa baraza kuu la jumuiya na taasisi za kiislamu Tanzania amewaasa viongozi wa madhehebu mbalimbali ya dini,kuacha kujiingiza katika vitendo viovu,visivyompendeza mwenyezi Mungu.

Hatua hiyo ya Sheikh Kundecha imekuja kutokana na kuibuka kwa vitendo viovu ikiwemo ubakaji na ulawiti wa watoto vinavyofanywa na baadhi ya viongozi wa dini.

Hakuna maoni