Zinazobamba

LATRA imelitaka shirika la Reli Nchini ( TRC) kuhakikisha linalinda usalama wa wananchi kwenye miundombinu ya reli mwendokasi SGR.

Mamlaka ya Udhibiti wa usafiri wa ardhini (LATRA) imelitaka shirika la Reli Nchini ( TRC) kuhakikisha linalinda usalama wa wananchi kwenye miundombinu ya reli mwendokasi SGR.

Kaimu Mwenyekiti Bodi ya Wakurugenzi LTRA  Henry Bantu.

Rai hiyo imetolewa leo na Kaimu Mwenyekiti Bodi ya Wakurugenzi LTRA  Henry Bantu katika ufunguzi wa maadhimisho ya wiki ya Usalama wa Reli yaliyofanyika jijini Dar es salaam.

Bantu amelisihi shirika hilo kuzingatia udalama wa wananchi katika maeneo ya miundombinu ya reli kwa kutoa elimu stahiki kwa wananchi wa mijini na vijijini ili waweze kufahamu alama mbalimbali za usalama zilizowekwa kwenye miundombinu ya reli hali inayoweza kusaidia kuepukana na ajari za treni.

Amesema kwamba shirika hilo liweke kitengo maalumu kitakachoshughulika na ulinzi na usalama ,miundombinu ya reli,abiria,pamoja na watumiaji wengine wa reli.

Amesema TRC iweke baadhi ya alama,ishara,na mambo muhimu ambayo mtumiaji wa reli anapaswa kuzingatia ili kuhakikisha mtumiaji wa reli anakua salama.
Mkurugenzi Mkuu wa shirika la reli Tanzania( TRC) Mhandisi Masanja Kadogosa.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa shirika la reli Tanzania( TRC) Mhandisi Masanja Kadogosa ameziomba halmashauri nchini kuwa na utaratibu wa kuishirikisha TRC kwenye utekelezaji wa miradi ya maendeleo ili kuweza kuepusha muingiliano wa miradi kati ya TRC na Halmadhauri hizo kwenye baadhi ya maeneo.

Kadogosa amesema kuwa katika maendeleo ya sekta ya reli nchini ,serikali imeweka fedha nyingi katika ukarabati na ujenzi wa miundombinu mipya ya reli ikiwemo ujenzi wa reli yankisasa SGR ili kuhakikisha usalama wa miundombinu ya reli kwa watumiaji ni lazima kuwepo kwa mikakati madhubuti ya kuhakikisha jamii inapata elimu ya usalama wa reli.

Pia amewataka wananchi katika makundi tofautitofauti ikiwemo wafugaji wanaochunga mifugo yao katika maeneo ya njia ya reli kuacha shughuli hizo za ufugaji katika maeneo hayo ili kuepusha ajari ambazo sio za laima.

Wengine aliowahusia ni walio na tabia ya kupiga picha katika njia za rele,kuegesha magari katika njia za reli,wanaosikiliz simu nakuweka visikiliza simu masikioni,wanaotembea,wanaokaa,wanaocheza na wale wanaoweka vitu vizito kwenye reli.

Katika maadhimisho hayo ya wiki ya usalama wa reli inayojumuisha nchi wanachama wa SADC chini ya umoja wa vyama vya reli kusini mwa afrika (SARA) inayoadhimishwa oktoba 10 kila mwaka,mwaka huu imekuja na kaulimbiu isemayo "Chukua tahadhali,Treni zina mwendo wa haraka,Ni hatari".

Kadogosa ameongeza kuwa tayari ujenzi wa SGR kutoka Dar es salaam kwenda Morogoro umekamilika kwa asilimia mia moja hivyo kwa sasa wapo katika majaribio.

Hakuna maoni