Zinazobamba

WATANZANIA WAMETAKIWA KUTUMIA VIWADUDU KUUA MAZALIA YA MBU,

WATANZANIA wametakiwa kutumia viwadudu kwa ajili ya kuua mazaria ya Mbu ili kufanikisha mapambano dhidi ya malaria

Rai hiyo imetolewa wilayani Kibaha mkoani pwani na Meneja wa uzalishaji wa kiwanda cha viwadudu mkoani hapa,Gasper Kimbi, ambapo amesema hatua hiyo itasaidia serikali katika kufanikisha mkakati wake wa utekelezaji wa kutokomeza mazalia hayo.

Amesema kulingana na mabadiliko ya TabiaNchi Mbu wengi kwa sasa hawang'ati tu usiku bali wanang'ata katika nyakati zote ikiwemo asubuhi, mchana na jioni hivyo ni wakati wa kutumia viwadudu hivyo kwa ajili ya kwenda kuua mazalia hayo.

"Tukishapunguza uzao wa Mbu,hawa mbu wanaoruka watapunga,na itapungua uwiano wa mtu kung'atwa itapungua tutaweza kuishinda maralia."Amesema Kimbi.

Aidha,Kimbi amesema teknolojia ya viwadudu inasaidia kuua Mbu katika mazalia hasa sehemu zenye madimbwi.

"Tukiwaua viruirui wa mbu,tunakuwa na uhakika uzao wa mbu tumeshaungamizi,hivyo jamii itumia teknoloji hii''amesema Kimbi.

Hakuna maoni