Zinazobamba

Jeshi la Polisi Kikosi Cha Usalama Barabarani limewataka madareva wanaofanya kazi serikalini kuzingatia sheria za Barabarani

Na Mussa Agustino

Jeshi la Polisi Kikosi Cha Usalama Barabarani limewataka madareva wanaofanya kazi serikalini kuzingatia sheria za Barabarani nakuacha tabia ya kudhani kuwa wapo juu ya sheria kwani wamekuwa wakisababisha ajari.

Hayo yamesemwa leo na Kamanda wa Kikosi Cha Usalama Barabarani Wilbroad Mutafungwa wakati wa Mafunzo ya siku moja Kwa Madereva wa Serikali yenye lengo la kuwakumbusha kutekeleza majukumu yao Kwa kuzingatia sheria za Barabarani Ili kupunguza ajali zinazojitokeza nakusababisha vifo na ulemevu wa kudumu.

"Nyinyi Madereva mnafanya kazi bila kuzingatia sheria japokuwa mmepata  Mafunzo kutoka katika vyuo vya usafirishaji vinavyotambulika kisheria,mmetahiniwa na kukabidhiwa chombo Cha moto Kwa mujibu wa sheria,lakini mmekuwa ni sehemu ya kusababisha ajari kutokana na kuzalau sheria za Barabarani nakujiona nyinyi mpo juu ya sheria" amesema Mutafungwa 

Aidha amesema kuwa asilimia 90 ya ajali zinazojitokeza zimekuwa zikisababishwa na tabia za Madereva kitokuzingatia sheria za Barabarani huku asilimia zingine za ajali zikisababishwa na masuala ya miundombinu ya Barabara na sababu zingine.
Mtafungwa amesema katika kipindi cha mwezi January 2022 hadi Agosti 2022 ajali zilikuwa 1,177 katika hizo ajali zilizotokana magari ya serikali 135 sawa na asilimia 11.5 huku jumla ya vifo vyote 11038 na 90 vilitokana na magari ya serikali sawa na asilimia 8 .7

Sambamba ya hayo amesema Majeruhi wote wa ajali walikuwa 1,556 walitokana na magari ya serikali 211 sawa na asilimia 13 .6 hivyo ajali ya magari ya serikali umekuwa siyo jambo la kustua imekuwa kawaida kwani asilimia kubwa hujisababishia wenyewe kutokana na viongozi kuwafanya Madereva wao wawe juu ya Sheria hawaonywi

Hakuna maoni