Zinazobamba

Kamati Ya Mdundo Wa Kitaifa Yaelekea Ukingoni Kukusanya Vionjo


 Mwenyekiti wa Kamati hiyo Dkt Kedmon Mapana ambaye pia ni Katibu Mtendaji Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) 

Na Mussa Augustine.

Kamati ya Mdundo wa Kitaifa iliyoundwa hivi karibuni na Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo  Mohamedi Mchengrwa imesema inaendelea na mchakato wa ukusanyaji wa maoni na Vionjo kutoka  katika mikoa ya Kanda zote nchini ili kusaidia  kupata Mdundo wa Kitaifa utakaoutumika kama  kitambulisho cha  taifa la Tanzania  .

Hayo yamesemwa leo Jijini Dar es Salaam na Mwenyekiti wa Kamati hiyo Dkt Kedmon Mapana ambaye pia ni Katibu Mtendaji Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) wakati akitoa mrejesho wa kazi iliyofanywa na kamati hiyo kwa muda wa miezi miwili tangu kuteuliwa kwake mwezi Julai Mwaka huu.

 Aidha Dkt.Mapana amesema kwamba miaka mingi Wanamuziki  wa Tanzania wamekuwa wakitumia mdundo ambao hauna asili ya Kitanzania ikiwemo “Piano” hali inayopelakea kukosa fursa ya kualikwa kwenye majukwaa ya muziki ya kimataifa .

 "Wanamuziki wa Kitanzania wamekuwa wakikosa kualikwa kwenye matamasha ya muziki kutoka mataifa ya nje  kutokana na nyimbo zao kukosa uhalisia wa mdundo wa asili kwani nyimbo nyingi wameigia mindundo ya nchi za Mangharibi"alisema Dkt Mapana

 Hata hivyo amesisitiza kuwa serikali inatarajia ndani ya miezi miwili iwe imeshakusanya maoni ya Watanzania kutoka makabila mbalimbali nchini huku wakishirikiana na kamati hiyo yenye wajumbe 13 ikiwemo waandaaji,waimbaji nguli wa muziki hapa nchini ili kusaidia kufikia lengo lililokusudiwa la kutengeneza mdundo wa kitaifa.

 Dkt Mapana amesema hatua hiyo ya ukusanyaji maoni na vionjo inaelekea ukingoni ambapo hivi sasa wako  mbioni kuhitimisha, nakwamba Midundo inaweza ikawa zaidi ya miwili ikitegemeana na maoni ya Watanzania kwani kutumika kwakwe hakutokuwa na masharti mengi na  itaruhusiwa kutumika ndani na nje ya Tanzania .

Naye Mmoja wa Wajumbe wa Kamati ya Mdundo wa Kitaifa ambaye pia  ni Mtangazaji nguli wa  TBC  Manju wa Muziki Bw.Masoud Masoud amesema Mdundo wa asili wa Kitaifa unaoandaliwa na Wizara ya Tamaduni,Sanaa na Michezo, utasaidia kumtambilisha mwanamuziki wa Kitanzania  popote anapokwenda na kupata fursa zinazotokea ambazo zilikuwa zinawapita kutokana na kuiga Midundo ya mataiafa mengine .

 " Hii inasaidia Wanamuziki wa Kitanzania kutambulika kutokana na Mdundo wa asili wa Kitaifa, na baadhi ya nchi za Afrika Mashariki ikiwemo Burundi,Uganda,Kenya,Rwanda ha ta kule Nigeria na Kongo wana Midundo yao ya Kitaifa ambayo inawasaidi kupata mialiko yakuenda kushiriki kwenye majukwaa ya muziki katika mataifa ya ulaya na Marekani" alisisitiza Masoud.


Hakuna maoni