Zinazobamba

Kikundi cha ASEDEVA kuadhimisha toleo la 3 la Marafiki Music Festival 2022

Kikundi cha Sanaa na Mziki cha ASEDEVA katika kuadhimisha toleo la 3 la Marafiki Music Festival 2022 kinatarajia kufanya shughuli mbalimbali za kijamii ikiwemo kufanya usafi katika Hospitali ya Mwananyamala na warsha ambayo itatoa elimu kuhusu biashara ya mziki.

Akizungumza na waandishi wa Habari leo Jijini Dar es Salaam Mkurugenzi wa ASEDEVA Isack Abeneko amesema tamasha hilo litafanyika Oktoba 6 hadi 8 2022 katika viwanja vya Makumbusho Village Museum Kijitonyama Jijini Dar es Salaam kwa matembezi ambayo yanalenga kuutangaza utamaduni wa Mtanzania.

Aidha amesema Marafiki Festival ni tamasha la kimataifa la muziki linalowaleta wasanii wa ndani na nje ya nchi kutumbuiza na kuonyesha uwezo wao wa kimuziki na hufanyika kila mwaka Oktoba Jijini Dar es Salaam na Bagamoyo.

Ameongeza kuwa tamasha hilo huwaleta wadau na wataalamu mbalimbali wa sanaa kubadilishana uzoefu na ujuzi wao na wasanii ili kuwajengea uwezo katika nyanja mbalimbali za sanaa na ubunifu.

Hata hivyo amesem kwa mwaka huu tamasha hilo ni sehemu ya mradi wa SANAAPRO unaofadhiliwa na Ubalozi wa Ufaransa nchini Tanzania na litashirikisha wanamuziki toka nchi mbalimbali ikiwemo Rwanda, Kenya, Zambia Uganda na Tanzania.

Kwa upande wake Muandaaji wa Singeli Festi Masudi Kandoro amesema kuwa tamasha hilo ni mojawapo mwa njia ya kuendelea kutangaza utamaduni wa Mtanzania ndani na nje ya nchi.

Aidha amesem kupitia tamasha hilo litawezesha kuwakutanisha na kuwaunganisha wasanii mbalimbali wa sanaa tofauti kujadiliana na kutoa mawazo yao ya njia bora za kuutangaza utamaduni wa Tanzania kutambulika hadi nje ya nchi

Hakuna maoni