Zinazobamba

Asasi ya HakiElimu Yazindua Utafiti wa Elimu Ya Uraia Shuleni

   Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Asasi ya HakiElimu Godfrey Bonvature

Na Mussa Augustine

Asasi ya HakiElimu imeishauri serikali kufanya mapitio ya Mtaala wa Elimu ya Uraia ili kutilia mkazo maudhui na mbinu za ufundishaji vinavyomwandaa kijana katika mawanda mapana ya ufahamu juu ya maana na umuhimu wa ushiriki wao katika madani za Siasa na Demokrasia.

Ushauri huo umetolewa na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Asasi hiyo Godfrey Bonvature wakati wa hafla ya uzinduzi wa ripoti ya Utafiti uliyofanywa na sasi hiyo mwaka 2022 kwa lengo la kuangalia mchango wa Elimu ya Uraia shule za Sekondari katika kumwandaa kijana kujifunza na kushiriki vema miachaka ya demokrasia Nchini.

Aidha amesema kwamba utafiti huo uliopewa jina la Mchakato wa” Elimu ya Uraia shule za Sekondari na Ushiriki wa Vijana katika Michakato ya Kidemokrasia Nchini”umeonesha kuwa elimu ya Uraia itolewayo shuleni ina mchango kidogo katika kumsaidia kijana wa kitanzania kujifunza na kushiriki shughuli za kisiasa na demokrasia.

“Asilimia 44.4 ya wanafunzi hawaelewi maana ya demokrasia ,aslimia 85.5 hawajawahi kushiriki au kushirikishwa katika vikao rasmi vya shule vinavyofanya maamuzi kuhusu mapato na mgawanyo wa rasilimali za shule ,huku asilimia 68.9 hawajawahi kugombea au kuonesha nia ya kugombea nafasi yoyote ya uongozi ngazi ya shule,ailimia 44 hawashiriki katika chaguzi za uongozi wa wanafunzi na asilimia 26hawajawahi kushiriki kabisa katika midahalo kama sehemu ya kuwajengea uwezo wa kuwashawishi na demokrasia”amesema Bonvature.

Katika Ngazi ya jamii utafiti huo umeonesha kuwa zaidi ya  asilimia 80 ya viajana walioshuleni hawajawahi wala hawajahamasishwa kushiriki mikutano ya kampeni na siasa ,hku asilimia 67.8 ya vijana hawajawahi kuhudhulia mikutano ya kijiji au mtaa na asilimia 67.5 hawajawahi kushiriki shughuli za kijamii zinazohusu maendeleo ya vijiji au mtaa kwa kujitolea.      

    Kamishna wa Elimu Dr.Lyabwene Mtahabwa

Kufuatia Utafiti huo Kamishna wa Elimu Dkt .Lyabwene Mtahabwa ameipongeza Asasi hiyo nakusema kwamba serikali ipo kwenye mchakato wa kupitia mitaala ya elimu ili kuwafanya vijana wanaohitimu masomo yao waweze kushiriki katika shughuli mbalimbali za maendeleo,hivyo serikali inaendelea kupokea maoni mbalimbali ya wadau wa elimu nchini.

“Serikali inaendelea na mpango wake wa kufanyia marekebisho sera ya elimu ili kuhakikisha vijana wetu wanaohitimu wapate elimu inayoweza kuwasaidia kushiriki kwnye shughuli za maendeleo,hata elimu ya uraia kwa vijana wetu ni muhimu sana kwani inawasaidia kushiriki kizalendo kwenye shughuli mbalimbali na kuiletea nchi maendeleo”amesema Dkt .Lyabwene.

Hata hivyo baadhi ya Wanafunzi waliohudhulia hafla hiyo wameiambia Fullhabari blog kuwa wamefurahishwa na Utafiti uliofanywa na Asasi ya HakiElimu kwani utasaidia kuisukuma serikali nakuona umuhimu wa kufanyia mapitio ya Mtaala wa elimu ya Urai Shuleni ili kuwasaidia vijana kushiriki katika shughuli za siasa na demokrasia,




Hakuna maoni