Zinazobamba

TGNP, Wildaf Kukinoa Chama cha CHAUMMA namna ya Kuandaa Sera ya Jinsia


Na. Vicent Macha 

Kukosekana kwa Wanawake katika ngazi mbalimbali za maamuazi kunasababisha kufanyika kwa maamuzi mengine ambayo si sahihi na yanakwenda kumuumiza Mwanamke moja kwa moja.

Picha ya pamoja baada ya mafunzo.

Hayo yameelezwa na Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA) Tanzania bara Bw. Youjin Kabendera wakati wa Mafunzo Maalum ya namna ya kuandaa Sera ya Jinsia, ambapo mafunzo hayo yanaendeshwa na Shirika la TGNP kwa kushirikiana na Wildaf Tanzania.

Bw. Kabendera amesema kuwa Sera ya Jinsia ni muhimu katika Taifa letu kwa kuwa inakwenda kulinda Haki za Mwanamke katika kufanya Siasa, na sisi kama CHAUMMA tunatamani kufanya siasa inayomshirikisha mwanamke moja kwa moja.

Aidha ameongeza kuwa takwaimu zinaonyesha kuwa Wanawake katika nchi hii ni wengi kuliko makundi yote lakini wamekuwa wakitimiwa vibaya na kuwa kama njia ya kuwapitisha wanasiasa kupata uongozi, na sisi kama CHAUMMA tunasema hatutakubaliana na hilo hivyo tunahitaji Wanawake wajitokeze kuja kugombea nafasi mbalimbali ndani ya Chama chetu katika nafasi yoyote ile.

Ameendelea kusisitiza kwa kusema kuwa si katika uongozi tu bali hata katika nafasi za Maamuzi tunatamani kuona wanawake wanakuwa wengi kuliko kundi lingine lolote, hivyo kwa wale wenye vigezo basi wajitokeze nasi tupo tayari kuwapokea.

Kwa upande wake Katibu wa jumuiya ya wanawake CHAUMMA Bi. Marry Mpangala ameshukuru sana TGNP pamoja na Wildaf kwa kuweza kuwaletea mafunzo hayo na kusema kuwa katika vyama vingi vya siasa ngazi za maamuzi zimekuwa zikishikiliwa na wanaume na wanawake wamekuwa wakiachiwa nafasi ndogo ndogo.

Ameongeza kwa kuwataka wanawake waje kwa wingi ndani ya CHAUMMA ili waweze kusogeza mbele Ajenda yao ya Ubwabwa na Maharage kuhakikisha inawafikia wangonjwa Mahosptalini na Watoto Mashuleni, na kuongeza kuwa wanawake wakati wa kujifungua wanapoteza damu nyingi hivyo wanahitaji chakula cha kutosha ambacho ni Ubwabwa na Mharage.

Nae Afisa Habari wa Chama hicho amejazia kwa kusema kuwa mafunzo hayo waliyoyapata watayafikisha kwa wanachama wao nchi nzima kuanzia chini kabisa katika Matawi, Kata hadi taifa ili waweze kufahamu umuhimu wa Mwanamke katika Uongozi.

Muwezeshaji wa Mafunzo Deo Temba akitoa maelekezo kwa Baadhi ya wajumbe wa CHAUMMA kuhusu namna ya kuandaa Sera ya Jinsia ya Chama hicho.

Baadhi ya Wajumbe wa CHAUMMA wakifuatilia mafunzo.
Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA) Tanzania bara Bw. Youjin Kabendera (Mwenye Tshirt Nyekundu) akitoa maoni yake katika zoezi la kuandaa Sera ya Jinsia ya chama hicho.

Hakuna maoni