Zinazobamba

Jaji Warioba Awataka Wanasiasa Kuacha Kuwagawa Watanzania

Na Mussa Augustine 

Jaji Mstaafu Joseph Sinde Warioba amewaomba viongozi wa kisiasa kuacha tabia ya kuwagawa wananchi nabadala yake waendeleze misingi iliyoachwa na muasisi wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ambaye alihimiza Amani,Umoja na Maendeleo.
Jaji Mstaafu Joseph Sinde Warioba.

Ombi hilo amelitoa leo Dar es Salaam kwenye kikao cha kubadilishana Uzoefu na Ujuzi kilichoandaliwa na Taasisi ya Mwalimu Nyerere nakuwakutanisha wadau mbalimbali ikiwemo viongozi wa vyama vya siasa,ambapo lengo kuu ni kujadili misingi iliyoachwa na viongozi wa Taifa tangu kupata uhuru mwaka 1961.

Jaji Warioba ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye kikao hicho amesema kwamba viongozi wa Taifa walifanya imani kuwa wananchi wote ni sawa ,nakwamba baada ya kupata uhuru viongozi hao  hawakuona umuhimu wa nchi kuwa huru huku wananchi wakiwa hawako huru,hivyo walihakikisha wanasimamia misingi ya Amani,Umoja na Maendeleo ili kulifanya Taifa la Tanzaia kuwa na Umoja.

"Baada ya Kupata uhuru mwaka 1961 viongozi wetu wa kitaifa walihakikisha wanaondoa ubaguzi wa Kikabila,Kidini  nakuamua kujenga Taifa la pamoja ,kipindi hicho tulikua tunaita nchi huru lakini wananchi hawana uhuru,hivyo wanasiasa wakubali msingi uliowekwa wa uhuru na amani,pia kuacha tabia ya vyama vya siasa kuwagawa wananchi" amesisitiza Jaji  Warioba ambaye pia ni  Mwenyekiti Mstaafu wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere.
Mwenyekiti wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere Joseph Butiku.
Awali Mwenyekiti wa Taasisi hiyo Joseph Butiku amesema kwamba Hayati baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere enzi ya uhai wake amekuwa akisimamia misingi ya Amani,Umoja na Maendeleo hivyo viongozi wa vyama vya siasa hawana budi kushirikiana kwa pamoja kuondoa changamoto zinazowakwaza watanzania katika kuwaletea maendeleo.
Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM ) Bara Christina Mndeme.
Nae Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM ) Bara Christina Mndeme , kando ya mkutano huo amewambia waandishi wa habari kuwa mdahalo huo ulioandaliwa na Taasisi ya Mwalimu Nyerere umewasaidia kupata mawazo ya namna yakuendeleza   misingi ya Amani,Umoja na Maendeleo iliyoachwa na Hayat baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Mkutano huo umewakutanisha viongozi mbalimbali ikiwemo viongozi wa siasa ,viongozi kutoka ofisi ya msajili wa vyama vya siasa,pamoja na kada mbalimbali ikiwa ni kubadilishana uzoefu na Ujuzi kuhusu misingi ya Amani,Umoja na Maendeleo.


Hakuna maoni