Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya HDT Dkt Piter Bujari (katikati)akisoma tamko la Taasisi hiyo kuelekea siku ya uchangiaji wa mfuko wa Global Fund.
Na Mussa Augustine.
Taasisi isiyo ya
kiserikali ya Health Promotion Tanzania ( HDT) imeiomba serikali ya Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania kuchangia Mfuko wa Global Fund kama nchi nyingine
zilivyoweza kujitoa kuchangia.
Ombi hilo limetolewa jana
na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo Dkt
Piter Bujari wakati akizungumza na Waandishi wa habari Jijini Dar es salaam
kuelekea siku ya uchangiaji wa Mfuko huo utakaofanyika Septemba 19 hadi 21
mwaka huu nchini Marekani nakubainisha kuwa
wakati sasa umewadia Tanzania
iahidi kuchangia kiasi cha fedha kwenye Mfuko huo.
Dkt Bujari amesema
kwamba Mfuko huo ni mahususi kwa kupambana na Ukimwi,Kifua Kikuu na Malaria
umeleta mafanikio makubwa Kwa nchi za Afrika ikiwemo Tanzania ,nakusisitiza
kwamba licha ya kupata msaada wa kutoka kwenye Mfuko huo umefika wakati
Tanzania na Nchi zingine za Afrika ambazo hazichangii Mfuko huo ziahidi
kuchangia kwa awamu hii ya saba .
Kwa mujibu wa taarifa
iliyotolewa na Dkt Bujari inasema kuwa kwa Afrika pekee nchi kama South
Africa,Kenya,Benini,Namibia,Senegal,Lesotho,Cote
D'Ivoire,Togo,na Zimbabwe,zimekua mstari wa mbele katika kuhakikisha nazo
zinachangia Mfuko huo,pia hivi karibuni Uganda iliahidi kiasi Cha Dola za
kimarekani milioni 6.
Aidha kupitia taarifa
hiyo iliyotolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa HDT Bujira imesema kuwa kidunia
Mkutano Mkuu wa Uchangiaji wa Mfuko kwa awamu ya saba utafanyika nchini
Marekani kuanzia tarehe 9 - 21 Septemba 2022 ,fedha hizi zinategemea kuokoa
maisha ya wanadamu zaidi ya milioni 20 Duniani kote ifikapo mwaka 2026.
"Kama ilivyotajwa
hapo juu Kwa miaka mitatu 2024-2026 kiasi kinachohitajika ni Dola za kimarekani
Bilioni 130 .2,ambapo Mfuko wa Global Fund watachangia Dola za Marekani
Bilioni 18 sawa na asilimi 14,vyanzo vya ndani Dola za Marekani bilioni 85.6 ,
Wafadhiri mbalimbali
wa Mfuko wa Global Fund wameahidi kiasi Cha Dola za kimarekani Bilioni 17 .5
ambapo mpaka sasa kiasi cha Dola za kimarekani Bilioni 16.6 zimeisha kusanywa
kati ya dola za kimarekani Bilioni 18 sawa na asilimia 92 zinazohitajika."
amesema Dkt Bujari.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya HDT Dkt Piter Bujari(mwenye suti) akiwa katika picha ya pamoja na waandishi wa habari huku wakiwa na mabango yenye ujumbe mbalimbali.
Aidha amesema kuwa kwa
Muda mrefu serikali ya Tanzania imekuwa ikishirikiana na Mfuko wa kimataifa wa
kupambana na Maradhi ya UKIMWI ,kifua Kikuu na Malaria katika kupanga na
kutekeleza afua mbalimbali za kupambana na Maradhi hayo ambapo Global Fund ni
Moja ya wafadhili wakubwa Duniani na Kwa nchi ya Tanzania katika kufikia
malengo ya sasa ya kutokomeza maambukizi mapya ya kifua Kikuu na virusi vya
UKIMWI ifikapo mwaka 2030.
Michango ya Global
Fund imesaidia kupunguza maambukizi mapya,kuwapatia matibabu wagonjwa na hivyo kupunguza
vifo na kuwawezesha wengi kushiriki shughuli za uzalishaji Mali na maendeleo ya
nchi kwa ujumla hata hivyo ugonjwa wa kifua Kikuu umeendelea kuwa tishio kubwa
nchini na Duniani kote ambapo vifo vitokanavyo na ugonjwa huo vimeongezeka Kwa
mwaka 2020.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni