Zinazobamba

Brela Yakutana na Wadau kusikiliza Maoini Juu ya Mabadiliko ya Sheria ya Leseni

Na Mussa Augusti

Wakala  wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) leo umekutana na wadau ili kusikiliza  maoni na mapendekezo yao juu ya mabadiliko ya Sheria ya Leseni za Biashara Sura 208 ya mwaka 1972 nakuangalia kama inatakiwa  kufanyiwa marekebisho au la.

Akizungumza na waandishi wa habari  Septemba Dar es Salaam kando ya kikako hicho Mkurugenzi wa Leseni kutoka BRELA Andrew Mkapa amesema maoni hayo yatafanyika kwa siku tatu kwa kukutanisha makundi tofauti.

Aidha Mkapa amesema kuwa  leo septemba 14 wameanza kwa kukutana na wadau kutoka taasisi mbalimbali za Serikali, huku kesho septemba 15 watakutana na watu wa Sekta Binafsi huku nakwamba keshokutwa ikiwa ni siku ya majumuisho ya maoni hayo kwa ajili ya kupelekwa kwa Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara kwa hatua nyingine.

“Nadhani wote mnafahamu kuna suala la leseni ya biashara ambapo wafanyabiashara wanapofanya biashara ni lazima wawe na leseni za biashara. Utoaji wa leseni ya Biashara unasimamiwa na Sheria ya Leseni ya Biashara sura 208,” amesema

Nakuongeza kuwa "BRELA ikiwa kama moja wapo ya mamlaka inayotoa hiyo leseni ya biashara, ilifanya mchakato wa kuwasiliana na Wizara Mama Wizara ya Uwekezaji Viwanda na Biashara ambayo Waziri wake ndiyo mwenya dhamana mama ya kusimamia Sheria hii, kwa ajili ya kufanya mabadiliko mbalimbali kwenye Sheria hii ili kuendana na wakati na mabadiliko yanayotokea,”.

Hivyo amesema kuwa sheria hiyo kama ilivyosheria kwa Sheria nyingine za nchi haitakiwi kuwa mgando inatakiwa kwenda na mabadiliko ya kisiasa, kiuchumi na kijamii yanayoendelea duniani na hapa nchini.

“Katika kufanya utekelezaji wa mabadidiko hayo, Wizara ya Viwanda na uwekezaji iliunda kikosi kazi ambacho kilikaa na kukusanya mapendekezo ya awali kwa ajili ya marekebisho ya sheria hii na baada ya kuwasilisha mapendekezo hayo Waziri Mwenye dhamana na Masuala ya Biashara aliagiza kwamba anataka kupata maoni ya wadau ambao kwa namna moja ama nyingine wanaitumia hii sheria,”.amesema Mkapa

Aidha Mkurugenzi huyo wa Leseni kutoka Brela amesema kuwa Kikako ambacho BRELA imekiandaa ni agizo la Waziri wa Uwekezaji na Viwanda na Biashara ili kuweza kupata maoni ya wadau ili kupata mapendekezo kwa ajili ya maboresho ya Sheria hiyo.


Hakuna maoni