Zinazobamba

Chongolo Awataka Makatibu Wa CCM Kusimamia Vizuri Mali Za Chama

 Na Mussa Augustine

Katibu Mku wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa Daniel Chongolo amewataka makatibu wa chama hicho kuanzia ngazi ya tawi hadi mkoa kuhakikisha wanasimamia vizuri mali za chama ili kukifanya chama hicho kuwa na maendeleo endelevu.

Chongolo alitoa agizo hilo jana wakati wa uwekaji wa majiwe ya msingi katika ujenzi wa ofisi ya CCM  Wilaya ya Kigamboni pamoja na Nyumba ya kuishi  Katibu wa CCM Mkoa wa Dar es salaam inayojengwa wilayani humo.

Alisema kwamba maafisa masuhuli wa chama pamoja na makatibu wanawajibu wakuhakikisha mali za chama zinakua salama hivyo kila mmoja anapaswa kuwajibika kulingana na majukumu yake kwenye nafasi aliyo nayo.

Pia alisema Chama kitawachukulia hatua za kisheria wale wote ambao watahusika katika kuhujumu mali za chama kwani chama hicho kina malengo makubwa ya kuwa na miradi mikubwa ambayo itasaidia kukifanya kiwe imara kiuchumi nasio  kutegemea wanachama wake kukichangia.

Katibu huyo wa CCM Taifa alisema kuwa kila kiongozi wa chama hususani makatibu ambao ndio watendaji wakuu watapimwa kwa vigezo ambavyo vinaendana na uwajibikaji wao nakwamba ambaye ataonekana kwenda kinyume na misingi ya chama atawajibishwa.

“Dhamana yakuwa  katibu sio dhamana bali kuna uwajibikaji nyuma yake,makatibu wote kuanzia ngazi ya tawi,kata,Ward,Wilaya,na Mkoa mimi ndio kiongozi wenu hivyo nawasihi mlinde mali za chama,na moja ya kigezo ambacho kitatumika kuwapima kwenye utendaji wenu ni utekelezaji wa yale yaliyoelekezwa kwenye sehemu ya nafasi yenu ya kazi”alisema.

Katika hatua nyingine Katibu Mkuu huyo wa CCM Taifa Daniel Chongolo alisema kuwa kumekuwa na tabia ya baadhi ya wanachma ambao wanatumia rushwa kwa ajili ya kupata dhamana ya uongozi ambapo amesema kuwa tabia hiyo haitafumbiwa macho nakwamba watakaobainika watachukuliwa hatua kali za kisheria.

Kauli hiyo ya Chongolo ilikuja kutokana na  hivi karibu uchaguzi wa viongozi ngazi ya wilaya ndani ya chama CCM uligubikwa na vitendo vya rushwa hadi kufikia uamuzi wa baadhi ya uchaguzi katika wilaya zipatazo 21 kufutwa na kurudiwa upywa,hata hivyo uchaguzi huo umekamilika siku ya alhamisi ya tarehe 20 mwezi huu.

“Bado tuna changamoto ya rushwa kwenye uchaguzi wetu ndani ya chama,tumemaliza uchaguzi ngazi ya wilaya macho yetu kwa sasa ni uchaguzi wa viongozi ngazi  ya mkoa ,macho yetu yapo wazi hatutasita kumchukulia hatua mgombea yeyote atakaebainika anatumia rushwa ili apate uongozi”alisema Chongolo.

Alisema kuwa Chama Cha Mapinduzi kina watu wasomi,wazuri,viongozi wenye mapenzi ya dhati na chama lakini tatizo ni baadhi yao kutengeneza miundombinu ya haramu ikiwemo rushwa ili  kuwadhibiti  wasipate dhamana yakuwa viongozi.

Awali akizungumza Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es salaam Mama Kate Kamba alisema kuwa mkoa wa Dar es salaam upo salama kutokana na ushirikiano wa viongozi wa chama  uliopo nakwamba viongozi hao watashirikiana ili kutekeleza vyenma ilani ya chama cha mapinduzi katika kuwaletea wananchi maendeleo.

Nae Katibu Chama Cha Mapinduzi(CCM) Mkoa wa Dar es Salaam Adam Ngalawa alisema kuwa ujenzi wa ofisi ya CCM wilaya ya Kigamboni unagharimu kiasi cha shilingi milioni 28196834 lakini mpaka sasa kiasi kilichotumika ni shilingi milioni 19731139,hivyo kiasi kinachohitajika ili kukamilisha ujenzi huo ni shilingi milioni 95363695,hata hivyo ofisi ya Katibu Mkuu CCM Taifa Danieli Chongolo tayari imechangia shilingi milioni 5 hadi sasa.

Alisema kuwa ujenzi wa nyumba hiyo tayari umefikia hatua ya umaliziaji na kwamba ujenzi wa Nyumba hiyo umeanza mwezi juni mwaka huu na unatarajiwa kukamilika mwezi desemba mwaka huu.

Hata hivyo baadhi ya viongozi na wadau mbalimbali wameahidi kuendelea kuchangia ujenzi huo ili kuweza kufanikisha kukamilisha haraka miradi hiyo.

 

Hakuna maoni