Simbachawene Azikumbusha Nchi za Maziwa Makuu Kuzingatia Uchaguzi Huru na Wahaki
Na Mussa Augustine.
Waziri wa
nchi ofisi Waziri Mkuu,Sera Bunge na Uratibu George Simba chawene amesema
kwamba nchi za Ukanda wa Maziwa Makuu zinapaswa kuona kuna haja ya kuwa na
uchaguzi huru na wahaki unaozingatia usawa kwa wote.
Waziri
Simbachawene amesema hayo leo Dar es salaam wakati akifungua wafunzo ya siku
nne yakujengea uwezo tume za uchaguzi na wadau wa uchaguzi wa jumuiya ya nchi
za ukanda wa maziwa makuu ICGLR.) ambapo mafunzo hayo ni sehemu ya itifaki ya
umoja wa mataifa(UN) inayohusiana na masuala ya Demokrasia na Utawala Bora.
Alisema kuwa
Tume za Uchaguzi za Nchi Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Nchi za Ukanda wa
Maziwa Makuu ( ICGLR) zitajadili namna ya kuboresha uadilifu na uchaguzi
unaoshirikisha makundi yote katika jamii kama vile wanawake ,
wazee,Vijana,na watu wenye ulemavu.
Alisema kuwa
matumizi ya TEHAMA katika uchaguzi pia yatajadiliwa,pamoja na fursa zilizopo
katika kuboresha ushiriki wa vijana katika uchaguzi ama kama wagombea au wapiga
kura ,ambapo pia wajumbe wa mkutano huo uanatarajia kujadili changamoto
na fursa zilizopo katika kuborsha suhiriki wa watu wenye ulemavu na wanaoishi
kwenye mazingira magumu katika chaguzi mbalimbali.
Waziri
Simbachawene aliendelea kusema kuwa Tume za Uchaguzi na Wadau wa Uchaguzi wa
Jumuiya ya Nchi za Ukanda wa Maziwa makuu ( ICGLR) zitahakikisha zinaondoa
changamoto ambazo zimekua zikisababisha kuwepo kwa siasa chafu na Demokrasi
isiyotoa haki sawa kwa makundi yote ikiwemo vijana na watu wenye ulemavu katika
kugombea nafasi mbalimbali za uchaguzi.
Alisema
kuwa hali ya kuwepo kwa Demokrasia safi husaidia nchi wanachama kuwa na
amani na Utulivu kwwenye mataifa yao,hali ambayo pia inasaidia kuondoa vifo
visivyo vya lazima vitokanavyo na masuala ya uchaguzi.
Kwa upande
wake Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguizi Tanzania NEC) Dkt
Charles Mahera alisema kuwa mafunzo hayo yatawasaidia kuwajengea uwezo wajumbe
na watendaji wa Tume za Uchaguzi za Jumuiya ya Nchi za Ukanda wa Maziwa Makuu.
Dkt Mahera
alizitaja Nchi kumi na mbili Wanachama wa Jumuiya ya ICGLR ni pamoja na
Tanzania,Angola,Burundi,Jamhuri ya Afrika ya Kati,Jamhuri ya Kongo,Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Kongo,Kenya,Uganda,Rwanda,Sudani Kusini ,Sudani na Zambia,
zikiwa na lengo wa kuhakikisha chaguzi zinakuwa huru,za haki na zenye kuaminika
ili kusaidia kukuza demokrasia itakayochochea amani , Usalama.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni