Zinazobamba

VETA yalenga kufikia vijana 700,000

 



Na Mwandishi wetu

Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) imeelezea nia yake ya kuwafikia watanzania laki saba (700,000) kuwapatia ujuzi wa ufundi ili waweze kujiajiri, malengo hayo ya miaka mitano.

 

Pia Mamlaka hiyo imejipanga kuanzisha mfumo wa mafunzo ya vitendo ambao utakwenda sambasamba na teknolojia ya viwanda.

Hayo yamebainishwa na MWENYEKITI wa Bodi ya VETA wakati akizungumza na waandishi wa habari sabasaba, kwenye maonyesho ya 46 yanayoendelea Viwanja vya Mwl. Nyerere Dar es Salaam

alisema, mafunzo hayo yatawasaidia wanafunzi kuweza kujiajiri wenyewe na si kusubiri kuajiriwa.



"Lengo letu ni kutaka kufikia vijana 700,000 ndani ya miaka mitano wapitie katika vyuo vyetu na kujipatia ujuzi wa aina mbalimbali,"amesema Dkt.Maduki.



Alisema, vijana hao watapitia mfumo wa mafunzo ya muda mrefu na muda mfupi na kupatiwa vyeti vyao.



"Na katika hao 700,000 hatutegemei waajiriwe bali wengine wajiajiri na kuzalisha ajira pia waweze kusaidia wawekezaji watakaokuja nchini,"amesema Dkt.Maduki.



Aidha, amesema VETA wamekuwa wakiwasaidia wale wanaofanya vizuri kwa kiwaungajisha na Tume ya Sayansi na Teknolojia (Costech) ili waweze kuendelezwa.



"Kwa mwaka jana peke yake tuliweza kusaidia wabunifu watano kuendelezwa na Costech,"amesema.



Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Veta Tanzania, Antony Kasore amesema wanazalisha nguvu kazi kulingana na sekta za kimkakati.

"Tunafundisha vijana namna ua kufanya kazi migodini, katika gesi ili wawezenkuwa msaada,"amesema Kasore

Hakuna maoni