VETA: ndizi Kitarasa ni muhimu kwa afya ya akili na kujenga mwili
Mkuu wa mafunzo ya huduma za ukarimu kutoka CHUO cha VETA cha Njiro Bw.Robinson Mwaikuju akionyesha Ndizi aina ya Kitarasa
Mkuu wa mafunzo ya huduma za ukarimu kutoka CHUO cha VETA cha Njiro akionyesha mkate wa Ndizi ya Kitarasa |
Zao la ndizi ni moja ya chakula muhimu sana katika baadhi ya mikoa hapa nchini, Nchini Tanzania mikoa inayoshughulika na kilimo cha ndizi kwa wingi ni pamoja na Kagera, Kilimanjaro, Mbeya, Arusha, Manyara, Mara, Tanga, Morogoro, Kigoma, na Pwani.
Zao la kitarasa
Ukienda mjini
Kilimanjaro, moja ya ndizi wanazozalisha kwa wingi ni ndizi aina ya Kitarasa,
zao hili limekuwa maarufu sana kutokana na utomvu wake. Licha ya ukweli kuwa
wanazalisha ndizi hizi, wengi wamekuwa hawazitumii kama chakula.
Sababu kubwa ya kutotumika
ndizi hizi ni utomvu wa ndizi hizi,kutokana na hali yake ya utomvu ndizi
zimekuwa na ukakasi sana wakati wa kula.
Ukiziona ndizi hizi zinatoa
utomvu mweupe, wakati mwingine unakuwa na rangi ya njano, hakika ni ndizi nzuri
lakini utomvu wake umekuwa kikwazo
Veta yajitosa kuhamasisha matumizi yake
Mkuu wa mafunzo ya huduma
za ukarimu kutoka CHUO cha VETA cha Njiro mkoani Arusha Robinson Mwaikuju,
amezungumza na mwandishi wa habari hizi akitaka kujua umuhimu wa zao hili na
juhudi wanazofanya kuhakikisha linasaidia jamii.
Mtaalam huyo wa mambo ya
vyakula, alisema zao la ndizi ya Kitarasa limejaaliwa mambo mengi, ni dhahabu
ya kijani ambayo bado watanzania hawajafanikiwa kuitumia ipasavyo.
Bw. Mwaikuju alisema,
Kitarasa inafaida nyingi katika mwili wa binadamu ikiwemo kutibu maradhi yasiyo
ambukiza.
Mtaalam huyo kutoka veta
Njiro ambacho kinamilikiwa na Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi(VETA)
aliwahimiza watanzania kupenda vya kwao hasa zao la ndizi Kitarasa.
“Zao la ndizi ya kitarasa
ni tiba ya kutibu magonjwa mbalimbali yakiwemo ya kisukari na presha,” alisema
Mtaalam huyo.
Kwa upande wake Mwanafunzi anayesomea katika
chuo hicho Happiness James Michael (Ngoko) alisema zao hilo lina faida kubwa
katika kujenga afya ya mwili na akili, pia inasaidia katika kupunguza hamu ya
kuvuta sigara.
Happines alisema kwa mtu
ambaye amekuwa na mazoea ya kuvuta sigara kwa wingi na amekuwa na nia ya kuacha
kuvuta, akitumia ndizi hizi kwa wingi anauhakika wa kuacha kabisa.
Mtalaam huyo ambaye
anasoma mwaka wa pili, ameshauri watoto kupatiwa uji wa ndizi ya kitarasa ili
kumsaidia kukua lakini pia watu wazima wameshauriwa kutumia zao hilo kwa
chakula.
“Hii ndizi ambayo
tumeileta hapa iko tofauti na ndizi zingine, zinaweza kutimu presha, magonjwa
ya moyo lakini pia inapunguza aroma,” alisema
Aidha akieleza kuhusu maonyesho
ya mwaka huu,Happy alisema wamekuja na kuonyesha watu umuhimu wa zao la ndizi
aina a kitarasa lakini pia mbaazi kwani mazao hayo ni dhahabu ambayo bado
haijatumika ipasavyo
“ukiangalia zao la ndizi
ya kitarasa na mbaazi zinakazi kubwa katika mwili wa binadamu, una fanya mambo
mengi kama unga wa ngano,” alisema.
Unaweza kutengeneza uji
kwa ajiri ya afya ya mtoto, unaweza kutengeneza mikate, bagia, keki na mifano
ya aina hiyo, vitu vyote hivyo ni muhimu kwa afya ya mwili.
“Kijijini bado wanatumia
bidhaa za zamani lakini kwa mijini bado kuna shida ya kuthamini vya kwetu, nataka
nikwambie zao hili la ndizi ya kitarasa ni dawa kwa afya ya watu, inaimarisha
akili na afya ya mwili,” alisisitiza
Vilevile alisema zao la
ndizi ya kitarasa ni zao ambalo halipewi kipaumbele katika matumizi, hivyo
wameona ni vizuri kuhamasisha jamii kulitumia.
“Hii ndizi unaweza
kutumia ikiwa mbivu, ikipikwa, na unga, lakini kwa sisi tulikuwa tunalenga
kutumia unga, hivyo tulikuwa tunachukua ndizi kitarasa kisha tunamenya
tunaanika na tukishaanika tunakwenda kusaga na kupata unga kwa ajili ya
matumizi ya kutengeza vile vitafunwa.
Chuo cha VETA Njiro kinatoa
maarifa na ujuzi mbalimbali ikiwemo uokaji mikate, keki na mapishi ya vyakula.
Pia inatoa ujuzi wa mapambo
na upambaji wa kumbi za starehe, mafunzo ya kompyuta na mbinu za uandaaji
Cocktail.
Kozi zingine ni usafi wa majengo na maeneo ya
wazi, huduma kwa wateja, mbinu za ujasiriamali, usimamizi wa shughuli za
mapokezi na vyumba.
Vilevile wanafundisha
ujuzi wa uhudumu na uuzaji wa chakula na vinywaji, uaandaji na upishi wa
chakula , utaalamu wa uongozaji watalii pamoja na uandaaji na uendeshaji wa
safari za watalii.
Ends,
Hakuna maoni
Chapisha Maoni