Zinazobamba

AZAM MEDIA LTD YAZINDUA TAMTHILIA TATU KWA MPIGO.

Na Mussa Augustine.

Azam Media Ltd kupitia msimu huu wa sikukuu imezindua tamthilia tatu kwa mpigo ili kuwapatia watazamaji  wake burudani isiyo kifani na kukonga nyoyo zao.

Akizungumza leo Desemba 3,2024 Jijini Dar es salaam wakati wa uzinduzi wa tamthilia hizo Msimamizi Mkuu wa chaneli ya  Sinema Zetu, Sophia Mgaza amezitaja tamthilia hizo kuwa ni Kombolea, Tufani pamoja na Kiki ambazo zimeandaliwa kwa ubunifu mkubwa.

"Tamthilia ya Tufani itaanza kuonyeshwa Deseamba 9,2024 siku ya jumatatu hadi Alhamisi saa 1:30 usiku,Kombolela itaanza kuonyeshwa Deseamba 13,2024 siku ya ,ijumaa hadi jumapili saa 1:00 usiku,huku tamthilia ya Kiki itaanza kuonyeshwa Desemba 16 ,2024 jumatatu hadi Alhamisi saa 1:00 usiku,ambapo tamthilia zote hizi zitaonekana kupitia chaneli namba 106 Sinema zetu HD" amesema Mgaza
Nakuongeza kuwa" Lengo la Azam Media Ltd kuendelea kutoa burudani ya hali ya juu kwa watazamaji Wetu huku tukisukuma Sanaa yetu kimataifa hasa katika nchi za kusini mwa jangwa la Sahara na popote.

Aidha amesema kuwa  Azam TV Max inawakaribisha watazamaji  kuungana nao msimu huu wa sikukuu huku wakiendelea kufurahi ofa ya kisimbuzi cha Antenna bure kwa kulipia kifurushi cha miezi miwili cha shilingi elfu ishirini na nane( 28000/= ) tu.
Aidha Mgaza amefafanua kuwa tamthilia hizo tatu ambazo ni Kombolela,Tufani na Kiki  zimewahusisha wakongwe wa uzalishaji wa filamu na tamthilia nchini pamoja na waigizaji nguli ,maarufu na wabobevu katika Sanaa ikiwa ni kutoa burudani ya aina yake kupitia Sanaa hiyo.

Akizungumza kando ya uzinduzi huo Jacob Steven maarufu kama  JB, amesema kuwa kwasasa soko la tasnia ya filamu na tamthilia linazidi kukua huku akiipongeza Azam Media Ltd kwa kuleta Mapinduzi makubwa kwenye tasnia hiyo ambayo imechangia kuleta ajira kwa Vijana wenye vipaji vya uigizaji.

Tamthilia ya Tufani imeandaliwa na Kampuni ya JB Film Company, huku tamthilia ya Kombolela imeandaliwa na Nabra Creative Company,ambapo Tamthilia ya Kiki imeandaliwa na Magazijuto Pictures.


Hakuna maoni