TIRA yajizatiti huduma bora, yaahidi kuwafikia 50% ya watanzania
Takwimu
ya miaka mitatu iliyopita inaonyesha kuwa watanzania zaidi ya 15% wanatumia
bidhaa mbalimbali za Bima hivyo mpaka kufikia mwaka 2023 Mamlaka ya usimamizi
wa Bima (TIRA) wamepanga kuwafikia watanzania kwa 50%.
Hayo aliyasema jana
Kamishna wa Bima Tanzania, Dkt. Baghayo Saqware wakati akizungumza na waandishi
wa habari akiwa katika Banda la TIRA katika maonesho ya 46 ya Biashara ya
sabasaba yanayoendelea Jijini Dar es Salaam.
Kwa upande mwingine Dkt.
Baghayo alisema Katika maonyesho ya sabasaba mwaka huu mamlaka ya usimamizi wa
Bima nchini (TIRA) kwa kushirikiana na watoa huduma wao makampuni ya Bima,
mawakala pamoja na washauri wa Bima wamekuja kutoa huduma mbalimbali za Bima
ikiwemo kuandikisha wanachama katika huduma za aina mbambali za Afya, Magari,
Nyumba, vifaa vya ndani na Biashara.
Pia Dkt. Baghayo alisema
katika maonyesho hayo ya sabasaba wanatoa leseni kwa mawakala ambao
wanaandikisha wanaotaka kujiunga kutoa huduma za Bima;
“Mamlaka imetoa miongozo
ya kusajili wauza Bima ambazo tunazo hapa na watu wote wanaweza kuja
kuzichukua, kuzisoma na kuangalia utaratibu wa kujisajili pamoja na miongozo ya
huduma tunamiongozo ya takaful ya makampuni yanayotaka kusajili”
Mbali na hayo Dkt.
Baghayo aliwashauri wananchi kukata Bima hasa bima binafsi ya Ajali ili
kujilinda zaidi kiafya;
“Katika mamlaka
tunashauri wananchi wanunue Bima zao binafsi, Bima za mtu mmoja wa tatu ni bima
ambayo mfaidika anakua hajawahi kukata Bima bali ni mtu mwingine ndiyo amekata
Bima, bima hiyo inaitaratibu fulani mrefu wa kuipata hivyo ni vizuri watanzania
wanaposafiri kutoka kituo kimoja kwenda kituo kingine wakate Bima binafsi za
ajali”
Aidha Dkt. Baghayo
aliwakaribisha wananchi wote Tanzania kutembelea banda la TIRA, makampuni ya
Bima, ofisi ya msuluhishi ili wapate taarifa mbalimbali ikiwemo ya
kujiandikisha, kutoa malalamiko au madai, na kusajili kampuni mpya ili
washiriki katika kuuza Bima
Hakuna maoni
Chapisha Maoni