Yanga yamsimamisha kazi anayedaiwa kuihujumu timu, ni wakili msomi Simon Patrick
Kaimu Katibu Mkuu wa mabingwa wa
kihistoria hapa nchini, Dar es Salaam Young Africa (Yanga) ambaye pia ni
Mkurugenzi wa Sheria na Wanachama, wakili Simon Patrick hatimaye amesimamishwa
kazi rasmi
Kwa mujibu wa taarifa iliyotangwa na
Mwenyekiti wa Kalabu hiyo, Mshindo Msola, alisema sababu za kumsimamisha
kuongozi huyo mwandamizi ni tuhuma za kuihujumu timu ya wananchi.
Maamuzi ya kusimamisha kazi Wakili
msomi Simoni Patrick umefanywa na kamati tendaji ya klabu ya Yanga kupitia
kikao chake walichofanya Novemba 17, 2020
Minong’ono ya wakili msomi Simon
Patrick kutimuliwa Yanga ilianza kusikika toka wiki iliyopita lakini viongozi
hawakuwa tayari kulitolea ufafanuzi suala hilo.
Kiongozi huyo anatajwa kuihujumu timu
hiyo kwa kutoa siri na kuzipeleka kwa wapinzani wao jambo ambalo linaweza
kukwamisha mikakati yao ya kutwaa ubingwa wa msimu huu wa Ligi Kuu Tanzania
Bara (VPL).
Tetesi zinadai kuwa kuanzia sasa
majukumu ya Wakili Patrick yatakuwa chini ya Mwenyekiti wa klabu hiyo Dkt. Mshindo
Msolla.
Yanga wameamua kufikia maamuzi hayo
baada ya kikao cha dharura cha Kamati ya Utendaji kilichokaa jana Novemba 17,
2020 ambacho kilifanyika maalum kwa ajili ya kusikiliza shutuma ambazo
amehusishwa nazo.
Kwa dhumuni la kuhakikisha haki
inatendeka, Kamati ya Utendaji itateua Kamati Huru kuchunguza swala hili na
kutoa maamuzi yenye tija kwa pande zote.
Hivyo, Kamati ya Utendaji itaisubiri
Kamati Huru kukamilisha uchunguzi wake na kutoa ripoti juu ya tuhuma hizi.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni