Viongozi wa CHADEMA wakamatwa kwa kuratibu maandamano
Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar
es Salaam, ACP Lazaro Mambosasa amesema wanawashikilia watu kadhaa
wakiwemo viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kwa
tuhuma za kupanga maandamano.
Viongozi wa Chadema wanaowashikilia
ni pamoja na mwenyekiti wa chama hicho taifa, Freeman Mbowe, Godbless
Lema, na Boniface Jacob aliyekuwa Meya wa Ubungo na mgombea ubunge wa
Jimbo la Ubungo.
Amesema wanawashikilia viongozi hao kwa kuwa
wanahatarisha usalama wa raia na mali zao kwa kuwa wamepanga kuanza
maandamano kitaifa yasiyokuwa na kikomo
Aidha, jeshi hilo
linaendelea kuwasaka watu wanaowashawishi vijana kushiriki maandamano
ambayo polisi wamesema ni ya vurugu. Wengine wanaosakwa ni viongozi wa
chama cha ACT Wazalendo.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni