Dk. Hsusein Mwinyi Aapishwa Kuwa Rais Wa Zanzibar
Viongozi
mbalimbali wa kitaifa wamehudhuria sherehe za kuapishwa kwa Rais mteule
wa Zanzibar, Dk Hussein Mwinyi ambaye amechaguliwa na wananchi wa
Zanzibar katika uchaguzi wa Oktoba 27 na 28.
Sherehe hizo
zimepambwa na gwaride maalumu la askari wa Jeshi la Wananchi (JWTZ),
Jeshi la Polisi sambamba na vijana wa halaiki waliokuwa wamekaa jukwaani
na kuvaa sare zenye rangi ya bendera ya Taifa.
Rais anayemaliza
muda wake, Dk Ali Mohamed Shein alikuwa kiongozi wa mwisho kuwasili
katika uwanja wa Amani ambako sherehe hizo zimefanyika na alielekea moja
kwa moja katika jukwaa maalumu ambapo alipigiwa mizinga 21 wakati wimbo
wa Taifa ukiimbwa.
Baada ya kupokea heshima hiyo ya mizinga,
askari walio katika uwanja huo walitengeneza umbo la Omega kama ishara
ya mwisho wa utawala wa kiongozi huyo, kisha akakagua gwaride hilo
likiwa kwenye umbo la Omega.
Wakati Rais Shein akikagua gwaride
hilo, helkopta ilipita juu ya uwanja wa Amani kama ishara ya kumuaga
kiongozi huyo ambaye amemaliza muda wake wa miaka 10 akiwa ni Rais wa
awamu ya saba katika visiwa hivyo.
Rais Shein alirejea katika
jukwaa la saluti na askari akashusha bendera ya Rais kama ishara ya
kukamilika kwa utawala wake. Baada ya kukamilika kwa kipengele hicho,
Rais Shein alipanda gari la wazi ambali lilisukumwa kuelekea kwenye
jukwaa maalumu kwa ajili ya kuapishwa kwa Rais mteule, Mwinyi.
Viongozi
wengine waliohudhuria hafla hiyo ni Makamu wa Rais, Samia Suluhu
Hassan, Waziri Mkuu, Kassimu Majaliwa, Makamu wa Pili wa Rais wa
Zanzibar, Seif Ali Iddi, Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Venance Mabeyo.
Wengine
ni marais wastaafu wa Tanzania, Ali Hassan Mwinyi na Jakaya
Kikwete,Makamu wa Rais mstaafu, Mohamed Ghalib Bilal, Waziri wa Mambo ya
Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Profesa Palamagamba Kabudi, Waziri wa
Mambo ya Ndani, George
Hakuna maoni
Chapisha Maoni