Sahau kuhusu Chama kwenda klabu ya Yanga, anamkataba na simba kwa miaka miwili na nusu-Dewji
"Ukweli ni kuwa Chama tumeshaini nae
mkataba atabaki na Simba hadi msimu wa 2022 kwahiyo ana msimu nusu na miaka
miwili imebaki, mimi kama Mwenyekiti siwezi kuja hapa kuongea mambo ya
uongo,"
Ni Kauli ya Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi
Simba, Mohammed Dewji wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu sakata
la kiungo Clatous Chama juu ya kubaki mitaa ya msimbazi.
Mohammed Dewji alisema kiungo, Clatous Chama
amesaini mkataba mpya kusalia klabuni hapo hadi 2022 na kufuta tetesi kuwa
huenda angeweza kuachana na miamba hiyo ya soka hapa Tanzania Mwishoni mwa msimu
huu.
Alisema baada ya kuwepo maneno mengi kuhusiana
na nyota huyo kuhusishwa na uhamisho wa kwenda Yanga wameamua kumuongezea
mkataba.
Kwa upande wake chama ambaye yupo nchi kwao
Zambia aliandika kupitia mtandao wake mananeno yakiashiria kuendelea kusalia samba.
“Taarifa
sijui anakwenda Yanga ni mambo ambayo si sahihi, hakuna sababu ya kuwa na hofu
na ninawatoa hofu mashabiki wa Simba kuwa tuko makini sana.
“Sehemu mbalimbali zimekuwa nikikutana na
mashabiki wa Simba ambao wananiambia Mo fanya Chama asiondoke Simba. Chama ni
mchezaji wa Simba.
“Suala kwamba anakwenda Yanga sijui linatoka
wapi lakini haina shida, sasa nimewaambia na ninafikiri leo tunafunga mjadala,”
alisema Mo Dewji.
Siku za karibuni kumekuwa na ripoti mbalimbali
zinazomhusisha Chama raia wa Zambia kuwa anamaliza mkataba wake mwezi Juni
mwakani hivyo anaweza akatua sehemu yoyote kama mchezaji huru lakini kutokana
na maneno ya Mo Dewji huenda tukaona Mwamba huyo wa Lusaka akiendelea
kukitumikia kikosi cha Wekundu wa Msimbazi Simba.
Post Comment
Hakuna maoni
Chapisha Maoni