Maadhimisho ya wiki ya magonjwa yasiyo ambukiza yafungwa rasmi, Kunenge awataka viongozi wa umma kuunganisha nguvu katika kuhamasiha jamii kujinga na maradhi hayo
Mkuu
wa Mkoa wa Dar es Salaam Aboubakar Kunenge ametoa wito kwa viongozi wa umma
kuhamasisha jamii ishiriki shughuli za nguvu, ikiwamo kufanya mazoezi kwa
takribani nusu saa kwa siku ili iweze kujikinga na maradhi ya magonjwa
yasioambukiza
Vilevile
amewwahasisha jamii kuzingatia mlo unaofaa hasa kwa kupunguza ulaji wa chumvi,
sukari, na Mafuta kwani vyote hivyo vinasababisha kuenena kwa magonjwa
yasioambukiza.
Pia
alisema kuondoa tatizo la magonjwa yasioambukiza yanahitaji nguvu ya pamoja
baina ya taasisi zote na wananchi kwa ujumla wake ili kuweza kuongeza nguvu ya
kuhakikisha magonjwa hayo yanapungua kwa kiasi kikubwa miongoni mwa watanzania.
Hayo
ameyabainisha mapema hii leo wakati akifunga wiki ya Maadhimisho ya Magonjwa yasiyoambukiza iliyoanza
Novemba 7, 2020 na kukamilika kwake leo Novemba 14, 2020 katika viwanja vya
mnazi mmoja.
Aliseama
jamii kwa umoja wao wanapaswa kuunganisha nguvu kuzuia Viatarishi vya magonjwa
yasioambukiza lakini pia kudhibiti matumizi ya vilevi kupita kiasi.
“Kwa pamoja inatupasa
tuunganishe nguvu zetu katika kuzuia viatarishi pamoja na kudhibiti matumizi ya
vilevi kama sigara na pombe na kuhamasisha kushiriki mazoezi” Amesema
Kunenge.
Aidha
Kunenge amewakumbusha wadau wote kuunda kamati ya pamoja ya uratibu wa Shughuli
zote za udhibiti wa Magonjwa yasiyoambukiza ilioagizwa na Waziri Mkuu wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Mjaliwa wakati wa awamu ya
kwanza ya uongozi wake ili kuweza kuwa na mwongozo wa pamoja katika kuandaa na
kutekeleza mipango na mikakati ya kitaifa kwenye udhibiti wa magonjwa haya.
“Nataka kuwakumbusha
mambo muhimu ya kuzingatia ili kujikinga na magonjwa yasiyoambukiza kwa kufanya
yafuatayo, kurekebisha ulaji wa vyakula kwa kuongeza ulaji wa mbogamboga,
matunda na kupunguza vyakula vyenye mafuta mengi, chumvi na sukari, kufanya
mazoezi angalau dakika 30 mara tano kila wiki, kuwa na utaratibu wa kupima afya
kila mara ili kuweza kupata matibabu mapema kabla ugonjwa haujaleta madhara
makubwa” ameshauri
Kunenge.
Maadhimisho
ya Wiki ya Magonjwa yasiyoambukiza hufanyika kila mwaka mwezi Novemba ambapo
mwaka huu yalizinduliwa Novemba 9,2020 na Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo
ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Prof. Mabula Mchembe na kuhitimishwa leo
Novemba 14,2020 kwa matembezi maalum yaliyoanzia viwanja vya Klabu
ya Leaders na Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kuelekea Viwanja vya mnazi mmoja
ambayo yalikuwa na kaulimbiu ya: “Wekeza
katika kukinga na kudhibiti Magonjwa yasiyoambukiza, Onyesha kwa Vitendo”
Hakuna maoni
Chapisha Maoni