Zinazobamba

Chanjo ugonjwa wa homa ya ini inapatikana kwa shilingi 20,000, wananchi watakiwa kujitokeza kuipata chanjo hiyo

 

Mratibu wa huduma tiba katika hospitali ya rufaa ya Mwananyamala Dkt Isdory Kiwale akizungumza na waandishi wa habari 




Mwandishi wetu

Wananchi wameshauliwa kujitokeza kwa wingi kupata chanjo ya homa ya ini inayotolewa katika hospitali ya rufaa ya Mwananyamala kwani kwa sasa huduma hiyo imepunguzwa gharama zake na wateja wanaweza kuhudumiwa kwa kiasi cha shilingi elfu 20,000 tu.

Akizungumza na waandishi wa habari katika viwanja vya mnazi mmoja Jijini Dar es Salaam Mratibu wa huduma tiba katika hospitali ya rufaa ya Mwananyamala Dkt Isdory Kiwale amesema magonjwa ya ini yana gharama kubwa katika matibabu yake hivyo ni vizuri kuwahi kupata chanjo yake.

“Sisi tunatoa chanjo kwa gharama ya shilingi 20,000 lakini wenzetu wanatoza zaidi ya hapo, hasa zile za binafsi, wanaanzia kuanzia 30,000, niwatie hamasa wananchi wa Wilaya ya Kinondoni wafike Hospitali ili kupatiwa chanjo hiyo” Dkt Kiwale.

Aidha akizungumzia wiki ya maadhimisho ya magonjwa yasioambukiza Mtaalamu huyo ambaye pia ni Daktari Bingwa wa upasuaji (Surgeon)  amekili kuwa bado kuna changamoto nyingi za magonjwa yasioambukiza na hivyo kuwataka watanzania kujibidisha kufanya mazoezi, kula mlo kamili, kuacha ulevi usio na tija na pia kuacha kuvuta sigara ambavyo vinachangia kwa asilimia kubwa tatizo la magonjwa yasioambukiza.

 


Hakuna maoni