Mtalaamu Regency awataka wananchi kujenga utamaduni wa kupima afya
Mkuu wa uendeshaji wa hospitali ya Regency, Bw. Om Josh akihudumia mteja katika wiki maadhimisho ya magonjwa yasioambukiza, yaliyofanyika viwanja vya mnazi mmoja Jijini Dar es salaam. |
Watendaji wa hospitali ya Regency wakiwa kazini katika banda lao, manzi mmoja mapema hii leo. |
Watendaji wakiendelea kutoa huduma. |
Na Mwandishi wetu
Hospitali ya Regency imewashauri watanzania kujenga tabia ya kuchunguza afya zao mara kwa mara ili kutambua hali zao kuliko kuendelea kusubiri hadi afya kuteteleka.
Akizungumza
katika kilele cha maadhisho ya wiki ya magonjwa yasioambukiza, Mtaalamu na Mkuu
wa uendeshaji wa hospitali ya Regency, Bw. Om Josh alisema tabia ya kusubili
mpaka kuzidiwa sio nzuri kwani inaweza kuhatarishia maisha.
Josh
ambaye alihudhuria pia katika viwanja vya manazi mmoja, alisema wiki ya
magonjwa yasioambukiza ilikwenda vizuri na hospitali yake pekee ilifanikiwa
kuwapima zaidi ya wananchi 1000, lakini alisisitiza ni vizuri wananchi
wakaendelea na utaratibu wa kupima afya mara kwa mara
“Tuko
hapa viwanja vya manazi mmoja toka Novemba 12, kwa kweli tumetoa elimu kubwa
kwa watanzania wenzetu, tumeweza kuwashauli na kuwapima watu 1000, tunataka
kuwaambia kuwa wanapaswa kubadilika wawe wanachunguza afya zao mara kwa mara,”
alisema Josh
Katika
hatua nyingine mtalaamu huyo wa huduma za afya amewataka vijana kujitokeza
kupima kwani kwa muda wote walioutumia katika viwanja hivyo vijana wamekawa na
mwitikio mdogo
“unaweza
kuwa na mwili mwembamba lakini bado unaweza kuwa na magonjwa yasioambukiza,
dawa pekee ni kujitokeza kupima ili kujua afya na kuchukua hatua stahiki,”
aliongeza
Aidha
akizungumzia sababu za vijana wengi siku hizi kukutwa na magonjwa
yasioambukiza, Mtaalamu huyo alisema kikubwa ni ulaji usio na tija,
Alisema
watu wengi wamekuwa wakijiachia sana, hawana muda wa kupanga lishe yao matokeo
yake wanajikuta wanakuwa na miili mikubwa na wengine kuwa na uzito uliopitiliza
na mwishowe kupata magonjwa yasiyoambukiza.
Vijana
wanajiachia sana, tuache tabia hizi, vinginevyo tutahatarisha afya zetu.
Takwimu za Shirika la Afya Duniani (WHO) zinaonesha kuwa
magonjwa yasiyoambukiza yanachangia zaidi ya vifo milioni 41 ambayo ni sawa na
asilimia 71 vya vifo vyote milioni 57 vilivyotokea mwaka 2016.
Vifo vinavyotokea nchini vinatokana zaidi na magonjwa ya
moyo na shikizo la Damu kwa asilimia 13, kisukari asilimia mbili, saratani
asilimia saba na ajali asilimia 11 hali hii kwa ujumla haikubaliki na
inatufanya tujumuike katika kujitathimini na kupanga mikakati ya pamoja.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni