Zinazobamba

Hassani Mwakinyo amempiga bondia muuza matikiti? mchekea-Wadau

 




Kuna hoja kwamba Bondia Carloz Paz Raia kutoka Nchini Agentina hakustahili kucheza mpambano na bondia namba moja  kwa ubora hapa Tanzania, Hassan Mwakinyo kwa kigezo kuwa Bondia Pazi tayari alishaonyesha kwa sasa sio bondia mzuri baada ya kukubali kupigwa mfulululizo mapambano mawili kwa KO  na mengine mawili kwa point.

Kitendo cha Bondia Mwakinyo Kupanda ulingoni na Bondia ambaye amezoea kupigwa huko nchini kwake ni ishara kuwa Tanzania inaandaa mapambano mremba kwa mabondia wao lengo ni kuwafanya wawe na majina na kisha watu kujipigia fedha kupitia migongo yao.

Imefika wakati, mapromota kuleta mabondia ambao wanathibitishwa ubora wao ulingoni lakini sio hawa ambao wameonekana kuwa ni mabondia mrenda mrenda.

 Tayari Mwakinyo amedhirisha ubiora wake hapa Bongo, tunahitaji kuona anacheza na watu ambao wanahistoria kubwa, lakini sio historia hizi za kushindwa mapema ambazo Bondia Carlos Paz anazimiliki.

 Akizungumza na Fullhabarionline, Mathian Nnunduma, alisema alikusomna kuona thamani ya mchezo wenyewe, muda mwingi Bondia kutoka Agentina alionekana kushindwa kuendana na kasi ya Mwakinyo, kwa bondia ngazo ya Basi hakutaratjiwa kuonyesha udhaifu raundi ya kwanza tu ya mpambano.

 

Aidha kwa upande wake, Abdallah Paz, kutoka Gongo la Mboto, akihojiwa na Fullhabarionline mara tu baada ya kumalizika kwa pambano, alisema mpambano ulikuwa mzuri lakini na Mwakinyo ameonekana kuendelea kubalika mechi baada ya mechi.

 

Pazi, alisema haikuwa kazi rahisi, kushinda mapema inaonyesha ni kwa jinsi gani, Mwakinyao alijiandaa na mpambano huo

“Tunajua bado Mwakinyo hajapambana na mtu yeyote hapa nchini, lakini alionyesha uwezo mkubwa katika pambano lake, na akiendelea kwa kasi hii basi anatafika mbali sana, tunaweza kumuona akiwa bingwa wa dunia kikubwa ni yeye kuendelea kufanya mazoezi.

 Bondia Hassan Mwakinyo ameshinda na kuetetea mkanda wake wa WBF Intercontinental Super Welterweight dhidi ya Carlos Paz raundi ya nne.

 

 


Hakuna maoni