Zinazobamba

Waislamu wagundua chanjo ya Covid-19






 ·       Ni Waturuki mume na mke

·       Watumia siku yao ya harusi maabara

New York, Marekani

Wakati vyombo vya habari vya Marekani vikitangaza kugunduliwa kwa chanjo mujarabu ya ugonjwa wa Covid-19 (corona), hakuna anayetangaza wavumbuzi hao ni nani.

 

Lakini kwa mujibu wa mtandao wa www.tattler.com, wavumbuzi wa chanjo hii iliyokuwa ikisubiriwa mno na ulimwengu mzima kumbe ni Waislamu tena mke na mume.

 

“It sounds like something out of an action film- a husband and wife scientists duo make a potentially life-changing breakthrough. Yet it is a reality for physician Ugur Sahin and Ozlem Turecci, the married couple responsible for the development of 90 per cent effective experimental covid-19 vaccine”,

 

Tafsiri: Inaonekana kama sinema ya kivita, wanasayansi wawili mke na mume wakifanya ugunduzi utakaobadili maisha ya watu. Lakini ndio uhalisia kwa daktari Ugur Sahin na Ozlem Turecci, mume na mke waliovumbua chanjo ya ugonjwa wa Covid-19 yenye mafanikio asilimia tisini.

 

Habari za kuweko kwa maendeleo mazuri ya chanjo mpya ya Covid-19 zilitangazwa kwa mara ya kwanza mnamo Novemba 9 mwaka huu.

 

Uvumbuzi huo chini ya makampuni mawili ya kutengeneza madawa ya binadamu, Pfilzer na BioNTech, ulieleza kwamba chanjo hiyo imewaponya watu tisa kati ya kumi.

Kutanagzwa huku kumepongezwa kama dalili y amatumaini katikati ya matukio ya mamilioni ya watu wanaogua na kufarikikwa ugonjwa wa Covid-19 huku Waziri Mkuu wa Uingereza, Boris Johnson, akisema nchi yake takuwa msitari wa mbele kupata chanjo hiyo.

 

Kwa mujibu wa gazeti Mailonline, Ugur Sahin mwenye umri wa miaka 55 ana asili ya Uturuki ni raia wa Ujerumani akifanya kazi kama Mkurugenzi Mkuu wa kampuni aliyoiunda yeye mwenyewe ya BioNTech nchini Ujerumani huku mkewe Ozlem Turecci akiwa mjumbe wa bodi ya kampuni hiyo nae pia ni Mturuki kwa asili.

 

Sahin alizaliwa Iskenderun nchini Uturuki na wazazi walihamia Ujerumani mwaka 1969 akiwa na umri wa miaka minne tu.  Wazazi wake waalikuwa wafanyakazi katika kiwanda cha kutengeneza Ford.

 

Sahin alisomea udaktari katika chuo kikuu cha Cologne na kuhitimu mwaka 1990 na kisha kupata shahada ya falsafa mwaka 1993.

 

Alifanya kazi katika hospotali ya Chuo Kikuu cha Saarland na mwaka 2000 akajiunga na Chuo Kikuu cha Mainz kabla ya kuwa Profesa na Mtafiti mwaka 2008 akifanya tahasusi katika masuala ya uvumbuzi wa chanjo za magonjwa mbali mbali.

 

Alimuoa mkewe Ozlem mwaka 2002 na hata siku ya ndoa yao baada ya kufunga ndoa waliendelea na utafiti wao maabara. Waliunda kampuni yao hiyo ya BioNTech ili kujishughulisha na vifaa tiba vya maradhi ya saratani.

 

Taasisi ya Bill na Melinda Gates iliwekeza Dola za KImarekani Milioni 55 katika kampuni ya wanandoa hao na kujikuta wakiwa miongoni mwa watu matajiri sana nchini Ujerumani. Kampuni hiyo pia inajishughulisha na maradhi ya kifu akikuu na Ukimwi.

 

Miongoni mwa uvumbuzi wao wa chanjo za maradhi mbali mbali, uvumbuzi huu wa chanjo ya Covid-19 ndio utakuwa mkubwa zaidi kwao kiasi kwamba watu mbali mbali wanashauri wawili hao wapewe tuzo ya Nobel katika tiba.

 

Watu wapatao milioni 55 ulimwenguni kote wamepata ugonjwa wa Covid-19 na idai ya vifo imefikia milioni moja na laki tatu hadi sasa.

 

Hapo ndipo umuhimu wa uvumbuzi wa Waislamu hawa wawili unapoonekana kwani chanjo hii itawezesha watu kupona na mataifa kufufua uchumi wao.

 

Ni fahari kwa Waislamu hawa mke na mume kuwa wavumbuzi wa chanjo ya Covid-19. Lakini kama kawaida hakuna anayetaja kuwa hawa ni Waislamu.

 

Ndiyo maana sisi Fullhabarionline tumeona tuandike kuhusu wavumbuzi hawa Waislamu waliouletea Uislamu heshima na pia iwe chachu kwa wataalamu mbali mbali wa Kiislamu kufanya kazi kwa bidii ili kuleta heshima kwa Uislamu na Waislamu duniani.

 


Hakuna maoni