Zinazobamba

Wafanyabiashara Arusha, Kilimanjaro waelekezwa kupitishia mizigo yao bandari ya Tanga



Mkurugenzi mkuu wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (PTA) Mhandisi Deusdedit Kakoko akizungumza na waaandishi wa habari Jijini Arusha (Hawapo pichani)juu ya matumizi sahihi ya bandari

 


 Na.Vero Ignatus Arusha.

Mkurugenzi mkuu wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (PTA)Deusdedit Kakoko,amesema kuwa kazi ambazo serikali inazifanya kupitia sekta  ndogo ya bandari, kupitia mpango wa tatu wa maendeleo wa miaka mitano ya bandari, ulioanza mwaka 2016/17, wameweza kupandisha mapato kutoka shilingi bilion 603, hadi takribani bil 951 katika mwaka 2019/2020,ikiwa ni  nyongeza ya takribani ya bil 70 kila mwaka.

Kakoko amesema Mamlaka hiyo imekuwa ikihakikisha kuwa shehena inaongezeka,ambapo mwaka 2016/17 shehena walizoweza waliyoweza kuihudumia ilikuwa tan mil 14.7,walipofunga mwezi june 2019/2020 waliweza kufikia shehena ya tan mil 17 .2 kwahiyo waliongeza tan mil 2.5 ,katika miaka mitano ya kipindi ambacho wanatekeleza mpango mkakati wao wa tatu wa miaka mitano, ikiwa na wastani wa nyongeza wa tani laki 5 kila mwaka.



 ''Mnaweza mkashangaa sana kwani  tumeweza kuhudumia takribani tan mil 17.2 walizohudumia takribani tan mil 11 ni za ndani tan mil 6 ndiyo za nchi za jirani na nawashukuru wananchi wa Tanzania  kwa kutumia bandari za Tanzania, ikiongozwa na ile ya Dar es salaam, hivyo nawashukuru wakurugenzi wa bodi ya TPA pamoja na menejimenti yote waliosaidiana nayo, zaidi rasilimali yetu kubwa ambayo ni wafanyakazi wetu''.alisema Kakoko.



 Mhandisi Kakoko alisema kuwa wakati wa nyuma bandari ya Tanga ilikuwa haifanyi kazi vizuri, kwani tani 300,000 za wafanyabiashara wa mikoa ya Tanga,kilimanjaro na Arusha zilikuwa zikipitia nchi ya jirani, ila kwa sasa kutokana na mabadiliko ambayo serikali ya tano iliweza kufanya wananchi na wafanyabiashara wameweza kuwarudishia tani 200,000,na wamebakisha tani 100,000,amesema wanapoitengeneza Tanga kutokana na gharama ilikuwa juu.



Alisema kuwa tayari Mamlaka hiyo ,wameshazungumza na wafanyabiashara kwamba watumie bandari hiyo ya Tanga, akiwemo mfanyabiashara A-Z wa mkoani Arusha ambaye baadhi ya makasha nusu  yanapitia nchi jirani,na nusu yanapitia Tanga,amewataka wafanyabiashara wa Arusha na Kilimanjaro ,wawe tayari kuitumia bandari hiyo kwasababu gharama zake zinakwenda kupungua na meli zinakwenda kupatikana



 Kakoko alisema kuwa wameweza kuipawisha mamlaka ya Bandari Tanzania ikaweza kutimiza wajibu wake, hadi kuwapelekea kuongoza kwenye gawio,ambapo katika  utekeleza jumla  katika mfumo wa biashara ya bandari alisema mfanyabiashara anaangalia mambo 3 muhimu ikiwemo gharama nafuu,muda uwe wa haraka na lazima kuwe hakuna usumbufu yaani kuwepo na ufanisi wa haraka .

 


Hakuna maoni