Nabii Dr Kennedy Mwasumbi awataka watanzania kuilinda Amani, aoteshwa mabasi matatu
Nabii wa Mwenyezi Mungu na muasisi wa huduma ya Tanzania Itubu Ministry (TIM) Dkt Kennedy Mwasumbi akizungumza na waandishi wa habari, hivi karibuni jijini Dar es salaam. |
Nabii wa huduma ya Tanzania Itubu Ministry (TIM) Dkt Kennedy Mwasumbi akifafanua jambo kwa waandishi wa habari. |
Na mwandishi
wetu
Nabii wa
Mwenyezi Mungu na muasisi wa huduma ya Tanzania Itubu Ministry (TIM) Dkt
Kennedy Mwasumbi amewashauri viongozi wa dini, serikali na vyama vya siasa
kuhakikisha kila mmoja anakuwa mstari wa mbele kulinda Amani ya nchi kwani
ikiharibika hakuna njia rahisi ya kuirejesha.
Alisema
hivi karibuni ameoteshwa na Mwenyezi Mungu juu ya habari ya Amani ya nchi,
ameonyeshwa mabasi matatu ambayo yalikuwa yanakaribiana kugongana katika
makutano, hiyo inaashiria kuwa wadu wa uchaguzi wasipokubaliana kwa kila mmoja
kucheza katika nafasi yake kuna uwezekano wa kutokea kwa machafuko katika
uchaguzi ujao.
Hayo ameyabainisha
Agost 16, 2020 wakati akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa Chikago
beach uliopo Mbezi Tangi Bovu Jijini Dar salaam.
Alisema katika
ndoto hiyo aliona mabasi matatu ambayo yaliandikwa majina, moja likiandikwa Serikali,
lingine likiandikwa Dini na la mwisho likiandikwa vyama vya siasa.
Aliyaona
mabasi hayo yakipita barabarani na mara yalipofika makutano ya njia ambako kuna
taa za barabarani, aliona yoote yakilazimisha kupita kwa wakati mmoja.
Kwa hofu
alifunga macho ili asione mabasi hayo yakigongana, alipokuja kufungua alikuta
kila basi limebakisha nafasi ndogo ili yagongane.
Aliendelea
lufafanua kuwa baada ya kuona hivyo, ikamlazimu kuuliza maana ya tukio hilo,
akaelezwa kuwa hiyo ni dalili kuwa kama watu hawatakuwa tayari kukubali matokeo
kuna uwezekano wa kutokea kwa machafuko katika nchi.
Alisema nafasi
ambayo imeachwa ni muda wa ziada ambao watanzania wanatakiwa kuutumia ili
kunusuru taifa kwa kuhubiri habari ya Amani lakini pia kuwashauri wadau wote wa
uchaguzi kukubali matokeo.
“Nimewaita
ili kuwaeleza unabii huu, mabasi hayo matatu yanamaana kubwa sana katika
unabii, nawashuari kila mmoja wetu kuomba Mungu ili aiweke nchi yetu katika
mikono salama, viongozi wa dini, vyama vya siasa na serikali wajitahidi kila
mmoja kuilinda Amani,” alisema
Kiongozi
huyo wa kiroho ambaye aliwahi kutabili
toka miaka ya 96 na utabiri wake ukatokea kweli aliwataka watanzania
kutopuuzia utabili wa wake kwani ni hakika damu itamwagika kama watu
wataavutana kama nilivyoona katika mabasi yale.
Dr
Mwasumbi, aliwahi kupata maono mwaka 1996 kuwa mvua kubwa ya elimino ingeweza
kunyesha hapa nchini Tanzania, utabiri wake ukaja kutimia mwaka 1998 ambapo
mvua kubwa ya kutisha ilinyesha.
Mbali na
hilo pia alitabiri ujio wa Rais John Pombe Magufuli, rais ambaye anachukia
rushwa, hatapanyi fedha, alipata maono juu ya utajili mkubwa katika taifa,
kutokana na hilo Mungu alimwambia nabii habari ya kuja kiongozi mwenye uchungu nan
chi hii, na mtendaji mzuri, hapo ndipo mashamba ya Tanzania yatakapoanza kutoa
mali za thamani kama vile mafuta, madini vitu ambavyo vilikuja kutokea.
Ends,
Maoni 3
Mungu atusaidie kwakweli
Mungu wa Mbinguni aendelee kuipigania nchi ya Tanzania
Barikiwa mtumishi
Hakika tunazidi kumwona Mungu wa Nabii Kennedy Mwasumbi kwa namna ya pekee sana hakika huyu ni nabii wa Mungu
Chapisha Maoni