Zinazobamba

CHUMU AWAOMBA WANAWAKE TEMEKE KUJITOKEZA KWA WINGI KUPIGA KURA ZA NDIO KWA AAFP OKTOBA 29 MWAKA HUU.


                 Chumu Abdallah Juma 

Na Mussa Augustine.Temeke ,Dar es salaam.

Mgombea mwenza wa urais kupitia Chama Cha Wakulima (AAFP)Chumu  Abdallah Juma amewaomba akina mama kujitokeza kwa wingi kukipigia kura za kishindo chama chake ili kiweze kushika dola nakuleta mabadiliko makubwa ya kiuchumi. 

Amesema hayo Septemba 17,2025 katika Viwanja vya  Mwembe yanga Wilayani Temeke Mkoani Dar es salaam wakati akijinadi kwa  Wananchi nakuwaomba kura za ndio,huku akisisitiza kuwa wanawake ni jeshi kubwa ambalo likiamua linaweza kuchagua kiongozi anayeweza kuleta mabadiliko makubwa ya kiuchumi katika jamii.
"Nawaomba sana Wanawake wenzangu tujitokeze tarehe 29 kukipigia kura za ndo chama cha AAFP,kwani sera zetu ni nzuri na zinalenga kuinua makundi yote mkiwemo nyinyi wakina mama wenzangu." amesema Mheshimiwa Chumu.

Nakusisitiza kwamba"nichagueni mimi(Chumu Abdallah Juma)mgombea mwenza,pamoja na Mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kunje Ngombale Mwiru,Wabunge na Madiwani wote wa AAFP ili tukasaidiane kuunda Serikali ambayo itakua na uchungu na rasilimali za nchi pamoja na kutatua kero zinazowakabili.
"Tumetembelea maeneo mbalimbali katika Wilaya ya Temeke nakuangalia changamoto zinazowapata Wananchi,tumeona mambo mengi ambayo bado yanatakiwa kufanyiwa maboresho ikiwemo upungufu wa huduma ya maji safi na salama,miundombinu mibovu ya masoko,hivyo mkitupa ridhaa chama chetu cha AAFP tutayafanyai marekebisho"amesema 

No comments