MHESHIMIWA MWIRU KUTUMIA KATIBA ILIYOPO KWA MIAKA MITANO YA URAIS WAKE.
*Asema suala la katiba mpya halitakua kipaumbele hadi wananchi wapate elimu.
*Lengo ni kuwaenzi waasisi wa katiba hiyo akiwemo hayati Nyerere,Mkapa, Mwinyi na rasi mstaafu Kikwete.
*Asisitiza huduma za kijamii kuimarisha nchi nzima.
*Walimu,Polisi na Waandishi wa habari kupewa kipaumbele.
Na Mussa Augustine.
Mheshimiwa Mwiru ametoa kauli hiyo Septemba 17,2025 katika Viwanja vya Mwembe yanga Wilaya ya Temeke Mkoani Dar es salaam nakubainisha kwamba wapo wagombea wa vyama vingine vya siasa ambao wanadanganya watanzania kwa kuwaahidi katiba mpya kila kukicha,wakidai endapo watashika dola suala la katiba mpya litakua ndani ya siku mia moja(100) au siku hamsini(50).
"Mimi lazima niwaenzi wazee wangu walioandaa katiba hii,sitashughulikia katiba mpya harakaharaka,katiba hii inataka elimu kwa wananchi,katiba ni roho ya watanzania,mtanzania huyu apewe shule ili aione katiba ya zamani aipitie,naya sasa aipitie ndio achukue maamuzi"amesema
Nakuongeza kuwa"Mimi nikiwa rais wa JMT nitawaenzi wazee wangu kwa ajili ya katiba,nitanzisha madarasa ya kueleimisha na kufundisha watu kuhusu katiba,mtanzania huyu anatakiwa akabidhiwe katiba mbili ile rasimu ya sasa na ile katiba ya zamani ili apitie,ajue katiba ipi inamfaa".
Aidha amesmea kuna baadhi ya watanzania ambao wanaibeza katiba iliyopo ambayo imeasisiwa na wazee wa nchi hiyo ya Tanzania akiwemo hayati Mwalimu Julius Nyerere,Ally Hassan Mwinyi, William Benjamin Mkapa,pamoja na rais mstaafu wa awamu ya nne Jakaya Mrisho Kikwete,pamoja na viongozi wengine waliopo.
*Huduma za Afya.
Amesema kua kuna changamoto kwenye masuala ya Afya kutokana na vituo vya Afya kukosa miundombinu mizuri pamoja na wahudumu wa vituo hivyo kutokuishi karibu na maeneo yao ya kazi ambapo akichaguliwa Oktoba 29 mwaka huu kua rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ndani ya mwaka mmoja atajenga nyumba za wahudumu wa Zahanati ili wawe karibu kutoa huduma.
*Changamoto za Walimu na Polisi.
Aidha amesema kuwa atasimamia changamoto za Walimu kwani wanafanya kazi kubwa kwani ndio waliofundisha mafisadi lakini wanaishi kwa shida,huku askari polisi wakilinda raia na mali zao,na bado wanaishi katika Mazingira magumu kutokana na mishahara yao kua midogo nakusema kua Serikali yake ya awamu ya saba itahakikisha ina mlinda Polisi na Mwalimu ili waishi kwenye Mazingira mazuri.
*Kitengo cha "Task Force" kufuatilia miradi yote ya ujenzi wa miradi.
Aidha amesema kuwa kitengo hicho kitakua na kazi ya kufuatilia ujenzi wa miradi ya umma,nakwamba Oktoba 29 mwaka akichaguliwa kua rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania atachimba bwawa la Mamba kwa ajili ya kutoa adhabu kwa mafisadi wote wanaokula fedha za umma.
*Makadirio ya Kodi kwa wafanyabiashara.
Amesema kuwa chama Cha Wakulima AAFP kitakua na makadirio yatakua madogo,lakini makusanyo ni lazima,nakulipa kodi ni thawabu,lakini kumekuwepo na watu wanaokwepa kulipa kodi kwa muda mrefu na wanadaiwa fedha nyingi za kodi,hivyo wadaiwa sugu watakutana na mamba Ikulu.
*Maiti kudaiwa.
Amesema kuwa hatovumilia madaktari wanaozuia maiti huku kuna mafisadi wanaendelea kutembea barabarani,nakwamba daktari atakaebainika kuzuia maiti ataingizwa mwenyewe kwenye jeneza.
"Hili ni Taifa lakizalendo lazima tuonane huruma,mtu ameuza mali zeke zote kumuuguza mgonjwa,bahati mbaya amefariki tena unamdai alipe deni la maiti,Serikali yangu haitokubaliana na hilo,maiti itachukuliwa bure" amesema
Nakuongeza kuwa" tumeshindwa kuweka mifumo yakinifu ya ukusanyaji wa Kodi bado tunang'ang'ania maiti,tuna vyanzo vingapi?.. tuna madini yamejaa,weeee Serikali yangu utakiona cha moto."
*Uzoaji wa taka.
Amesema kua uzoaji wa taka utakua ni bure nchi nzima kwani kila mtaa ataweka Lori la kukusanya taka na Wananchi hawatatizwa fedha yoyote
"Haiwezekani hata takataka watu wanageuza Mradi,watu wanagongewa asubuhi watoe taka na hela huku risiti zenyewe hazitolewi kwa mashine zinandikwa kwa mkono,Serikali yangu haitokua Tayari kwa hilo".amesema Mheshimiwa Kunje.
Nakuongeza kuwa lengo kubwa la Serikali yake ya mchakamchaka Baraza lake la Mawaziri halitazidi Mawaziri kumi na watano(15) pamoja na Mawaziri kivuli kumi na tano(15)kwa ajili ya kubana matumizi lakini baraza hilo litafanya kazi utadhani kuna Mawaziri 200, nakuleta maendeleo ya haraka naya lazima.
*Waandishi wa habari wakumbukwa.
Mheshimiwa Mwiru amesema kuwa Waandishi wa habari wamekua kikoo kikubwa duniani,wana uwezo wa kutumia kalamu yao kama silaha ya kuchonganisha nchi,nakwamba Serikali yeke wanahabari watembee kifua mbele kwani atawawezesha kwa nguvu zote watembee Vijijini wakachukue changamoto zote wazete Ikulu.
*Wahamiaji haramu.
Wanaingia watu wengine ambao wana maadili ya kishenzi halafu baadae Watanzania wenyewe wanalalamika kua nchi haina maadili na uzalendo mpaka wanaume wanamziki wanaovaa hereni kwani hawa wamejifunza wapi hapa kwetu?....maadili yetu ya kuvaa hereni mwanaume?...na ndio maana nimesema mwanamziki yeyote atakaevaa hereni mwanaume viboko 12 pale Ikulu.
*Kujenga Madarasa maalumu ya kufundisha Uzalendo na Maadili.
Aidha amesema kuwa Serikali yake itajenga madarasa kila kata nakutumia wastaafu waliofanya kazi Serikali ambao bado wana hali nzuri ya kiafya na watalipwa kima cha chini cha mshahara kwa ajili ya kufundisha Uzalendo na Maadili kwa wananchi.
*Mashekh na Wachungaji kwaheri kwenye siasa.
Amesema kuwa kuna baadhi ya viongozi wa dini ambao ni mashekh na Wachungaji wamekua wakijitokeza kugombea nafasi mbalimbali za Kisiasa ikiwemo udiwani na Ubunge nakusisitiza kuwa Serikali yake haitoruhusu kiongozi yeyote kuingia kwenye siasa bali andeleze maono yake ya kiro kwa wamini wake.
No comments
Post a Comment