Zinazobamba

MAOKOLA AKUMBUSHA MRADI WA FREMU ZA MADUKA KWENYE HIFADHI YA BARABARA.


                        Rashid Maokola 

Na Mussa Augustine.

Katibu mwenezi wa chama Cha Wakulima ( AAFP) Rashid Maokola amewaomba mgombea ubunge jimbo la Mbagala Ndonge Said Ndonge endapo akipewa ridhaa ya kua mbunge wa Jimbo hilo afuatiliea 
mradi wa ujenzi wa fremu zilizojengwa kwenye hifadhi ya barabara ya Mwendokasi Mbagala.

Amesema hayo Septemba 15,2025 Temeke Jijini Dar es salaam wakati akiwanadi na kuwaombea kura za ndio kwa Wananchi wagombea wa Ubunge Jimbo la Temeke Yusuph Rai pamoja na mgombea Udiwani kata ya Tandika Salum Tindwa "Kibuda" ,ikiwa ni muendelezo wa kampeni za uchaguzi mkuu za chama hicho  zinazoendelea nakwamba Mamlaka ya kudhibiti na kupambana na rushwa (TAKUKURU?Wilaya ya Temeke hadi sasa haijatoa majibu yoyote licha ya taarifa yake ya awali kua inafuatilia ujenzi wa fremu hizo.

Maokola amewambia Wananchi kua  fremu  hizo zimejengwa kwenye  eneo la barabara ya Chamazi-Kongowe ambapo umepita mfereji wa Maji taka,Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano pamoja na kituo cha Mabasi ya Mwendokasi lakini Serikali ya CCM imekaa kimya.
Aidha amesema kua Serikali ya AAFP itakua na jukumu kubwa kupitia viongozi wake wa jimbo la Mbagala kupambana usiku na mchana kuzuia mradi huo kwani una athari kubwa kwa Watanzania.

"Mimi ni Mwananchi wa kawaida kabisa,shida zote za Mbagala nazifahamu,lakini nimeona wakati wa uchaguzi nisibaki tu kua vilevile basi niwe Mgombea kwasababu hakuna mtu mwingine anayeweza kusawazisha zile shida,nawambia Wananchi wenzangu wa Mbagala mti dawa(Mbunge)unakuja tuchaguane sisi wenyewe Wananchi tuachane na habari za viongozi,viongozi hawajatufikisha pale sisi tunapotaka." amesema Maokola 
Ameendelea kusema kuwa Mbagala kuna kero nyingi ikiwemo Miundombinu ya Barabara,nakwamba Wananchi  wa Mbagala wanao fanya Biashara zao barabarani wanafukuzwa,lakini kuna Mwekezaji kajenga fremu za biashara katika kituo cha Mwendokasi kinyume na taratibu bila kuchukuliwa hatua zozote za kisheria. 

Nakusisitiza kuwa"Lazima tuhakikishe kwamba kama sisi wafanyabiashara tunatoka barabarani basi tunaenda kuweka pale mbele ya fremu na tusione mgambo au mtu yeyote kwasababu anaekaa kwenye fremu anafanya makosa na aliyetandaza biashara zake pale barabarani anafanya makosa,wana Mbagala tushikamane matatizo yetu hakuna mtu mwingine ambaye atakuja kututatulia,tuachane na habari za viongozi.

No comments