UZINDUZI WA KAMPENI ZA MGOMBEA UBUNGE AAFP JIMBO LA TEMEKE BALAA.
*Wananchi Tandika wa mlaki kwa shangwe na ndelemo.
*Awaahidi makubwa endapo watampa ridhaa kua Mbunge wao.
*Wao wasema ni kijana mwenye uwezo na maono makubwa ya kuwapigania kimaendeleo.
*Wamuahidi Septemba 29,2025 njia yake ya kwenda bungeni ni nyeupe.
Na Mussa Augustine.
Rai amesema hayo Septemba 15,2025 wakati akihotubia mamia ya Wananchi waliofurika kwenye uzinduzi wa kampeni za ubunge jimbo la Temeke kupitia chama hicho,nakuwaomba Wananchi wampigie kura za kishindo yeye na Mgombea udiwani wa kata ya Tandika kwa tiketi ya chama hicho Salum Abdallah Tindwa"Kibuda" ili wasaidiane kuhimiza shughuli za maendeleo.
Amesema Rai kua kumekua na viongozi kwenye jimbo la Temeke ambao wanapendwa,wanashangiliwa na kuungwa mkono lakini wakipata uongozi kwenye jimbo hilo wanaenda kufanya mambo yao binafsi na sio mambo ya Wananchi wa Temeke.
"Nikaona hapana ninao uwezo mkubwa wa kuomba ridhaa kwa Wananchi wa jimbo la Temeke,wanaweze kunichagua ili niende nikaongoze kwa niaba yao na sio kwa niaba yangu na chama chagu".amesema
Nakuongeza kwamba"ndugu zangu nataka niwambie CCM sio mbaya wabaya ni watu wake, kwasababu kwa miaka zaidi ya sitini tumekua tuna waamini watu ambao wanatokana na chama cha Mapinduzi,wengine ni marafiki zetu,wengine ni ndugu zetu,lakini wakipata uongozi chama kina wabadilisha."
Yusuph Rai ambaye pia ni mwenyekiti wa baraza la Vijana AAFP ngazi ya Taifa amesema kua madhumuni ya kugombea ubunge jimbo la Temeke nikwenda kuzungumza yale Wananchi wamemtuma, huku akisisitiza kua yupo tayari kupambana kurudisha hadhi ya Wilaya ya Temeke.
"Watu wanasema Wilaya ya Temeke ni Wilaya dume,sio tu kwa wingi wa watu au wapiga kura,lakini Wilaya ya Temeke ndio jimbo lenye wawekezaji wengi kuliko Wilaya zote Mkoani Dar es salaam."amesema
Mgombea ubunge huyo amesema kuwa wilaya Temeke ina wawekezaji wengi,Matajiri wengi na Wananchi wengi lakini haina hadhi kimaenendeleo.
Amesema kua jimbo la Temeke ndo jimbo pekee ambalo lina Viwanda vingi na idadi kubwa ya wapiga kura kuliko jimbo lolote katika Mkoa wa Dar es Salaam,lakini pia lina watu makini.
Halikadhalika amesema jimbo la Temeke limeongozwa na vyama vya siasa ambavyo ni CCM,NCCR-Mageuzi,CUF,na sasa ni yake kwenda kufanya maamuzi ya kupata kiongozi anaetokana na chama cha wakulima(AAFP).
Akizungumzia changamoto za Maendeleo jimboni humo,Yusuph Rai amesema jumbo la Temeke lina changamoto nyingi ambazo akichaguliwa kua Mbunge wa Jimbo hilo septemba 29 mwaka huu atazitatua.
Aidha amezitaja changamoto hizo kua ni pamoja na miundombinu ya Elimu, barabara,ukusanyaji wa taka,huduma za Maji safi na salama huku akiahidi kua ataziondoa mara moja akiwa Mbunge wa Jimbo la Temeke.
*Elimu bure.
Amesema jimbo la Temeke lina shule chache za sekondari na kidato cha tano na sita,nakwamba akichaguliwa kua Mbunge wa Jimbo hilo ataenda kupiga kelele kwenye bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwamba inatakiwa miundombinu ya ghorofa kwenye maeneo shule zote kwasabubu Vijana wanaopata Elimu ni wengi kuliko miundombinu ya majengo ndani ya jimbo hilo.
Kuhusu mtoto mwanafunzi kutozwa gharama mbalimbali ikiwemo pesa ya mtihani kila mara Mheshimiwa Yusuph Rai amesema kuwa akiwa Mbunge wa Jimbo hilo atapambana kuondoa hali ya kuchangishwa Wazazi kwenye shule ambazo zinatakiwa kutoa elimu bure.
Pia amesema kua jimbo la Temeke limekua na ufaulu duni wa wanafunzi kutokana na uwezo wa walimu waliopo kua mdogo,nakwamba akipata ridhaa ya kua Mbunge atahakikisha walimu wote wanachujwa nakupata walimu wenye uwezo wa kufanya wanafunzi wanafaulu kwa kiwango kizuri .
*Uzoaji wa taka.
Aidha amewambia Wananchi wa Wilaya ya Temeke kua kuna changamoto ya wakandarasi wa kuzoa taka kutokana na wazabuni waliopewa tenda hizo kua na uwezo mdogo wa vitendea kazi,huku wakikusanya fedha kwa Wananchi huku taka hizo zikiwa zinasababisha harufu mbaya na magonjwa ya mripuko.
"Mkinichagua kua Mbunge wa jimbo la Temeke,kwanza kupitia mfuko wa Jimbo,lakini pia nitazungumza na wawekezaji wa jimbo la Temeke ili kuhakikisha kila kata katika kata zote 13 tunahakikisha ya kwamba tunapata gari moja ambalo litazoa taka zote bure kwenye kata zetu" amesema.
*Maji safi na salama.
Amesema kua ni aibu kubwa kwa kata ya Tandika kukosa Maji safi na salama nakuahidi kwamba akichaguliwa na Wananchi kua Mbuge wa Jimbo la Temeke ataenda kupiga kelele kwenye Wizara ya Maji ili ilete magari ya kuchimba visima vya Maji kwa Wananchi wa Tandika na maeneo mengine jimboni humo wapate huduma ya Maji safi na salama.
*Soko la Tandika kua la Kimataifa.
Rai amewambia Wananchi kua Soko la Tandika linatakiwa liwe soko la Kimataifa kama lilivyo soko la Kariakoo kwa sasa kutokana na kuwepo kwa mzunguko mkubwa wa biashara na wingi wa wananchi wanaokwenda kupata huduma sokoni hapo.
"Tunazo Kariakoo mbili,Kariakoo ya Ilala na Kariakoo ya Temeke,unaposema Kariakoo ya Temeke ni Tandika,leo hii Tandika soko lake limekua kubwa la kibiashara,nikiwa Mbunge nitaenda kuishawishi Serikali ili tutumie soko hili tulibadilishe liwe la Kimataifa na sio soko la Wilaya,."amesema..
*Kituo cha daladala Temeke.
Mgombea huyo wa ubunge kupitia Chama Cha Cha Wakulima(AAFP) Yusuph Rai amesema kua eneo la Serikali lililopo Temeke mwisho atahakikisha linatengwa kutengeneza kituo kikubwa Cha daladala,chenye hadhi na thamani ya Wilaya ya Temeke,kata ya Tandika na jimbo la Temeke kwa ujumla.
" Kituo hiki kitaunganisha magari kutoka a Kariakaoo na yanayoenda kusini ili kuongeza thamani ya pato,mama lishe wafanye biashara pale, bodaboda wafanye biashara pale, daladala wafanye biashara pale,wabeba mizigo watabeba,wageni wataingia,kwa maana hivyo tutaongeza kipato ndani ya jimbo letu(Temeke)" amesisitiza
No comments
Post a Comment