Zinazobamba

Nabii Dr Kennedy Mwasumbi awataka watanzania kuilinda Amani, aoteshwa mabasi matatu

 

Nabii wa Mwenyezi Mungu na muasisi wa huduma ya Tanzania Itubu Ministry (TIM) Dkt Kennedy Mwasumbi akizungumza na waandishi wa habari, hivi karibuni jijini Dar es salaam.



Nabii wa huduma ya Tanzania Itubu Ministry (TIM) Dkt Kennedy Mwasumbi akifafanua jambo kwa waandishi wa habari.




Na mwandishi wetu

Nabii wa Mwenyezi Mungu na muasisi wa huduma ya Tanzania Itubu Ministry (TIM) Dkt Kennedy Mwasumbi amewashauri viongozi wa dini, serikali na vyama vya siasa kuhakikisha kila mmoja anakuwa mstari wa mbele kulinda Amani ya nchi kwani ikiharibika hakuna njia rahisi ya kuirejesha.

Alisema hivi karibuni ameoteshwa na Mwenyezi Mungu juu ya habari ya Amani ya nchi, ameonyeshwa mabasi matatu ambayo yalikuwa yanakaribiana kugongana katika makutano, hiyo inaashiria kuwa wadu wa uchaguzi wasipokubaliana kwa kila mmoja kucheza katika nafasi yake kuna uwezekano wa kutokea kwa machafuko katika uchaguzi ujao.

Hayo ameyabainisha Agost 16, 2020 wakati akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa Chikago beach uliopo Mbezi Tangi Bovu Jijini Dar salaam.

Alisema katika ndoto hiyo aliona mabasi matatu ambayo yaliandikwa majina, moja likiandikwa Serikali, lingine likiandikwa Dini na la mwisho likiandikwa vyama vya siasa.

Aliyaona mabasi hayo yakipita barabarani na mara yalipofika makutano ya njia ambako kuna taa za barabarani, aliona yoote yakilazimisha kupita kwa wakati mmoja.

Kwa hofu alifunga macho ili asione mabasi hayo yakigongana, alipokuja kufungua alikuta kila basi limebakisha nafasi ndogo ili yagongane.

Aliendelea lufafanua kuwa baada ya kuona hivyo, ikamlazimu kuuliza maana ya tukio hilo, akaelezwa kuwa hiyo ni dalili kuwa kama watu hawatakuwa tayari kukubali matokeo kuna uwezekano wa kutokea kwa machafuko katika nchi.

Alisema nafasi ambayo imeachwa ni muda wa ziada ambao watanzania wanatakiwa kuutumia ili kunusuru taifa kwa kuhubiri habari ya Amani lakini pia kuwashauri wadau wote wa uchaguzi kukubali matokeo.

“Nimewaita ili kuwaeleza unabii huu, mabasi hayo matatu yanamaana kubwa sana katika unabii, nawashuari kila mmoja wetu kuomba Mungu ili aiweke nchi yetu katika mikono salama, viongozi wa dini, vyama vya siasa na serikali wajitahidi kila mmoja kuilinda Amani,” alisema

Kiongozi huyo wa kiroho ambaye aliwahi kutabili  toka miaka ya 96 na utabiri wake ukatokea kweli aliwataka watanzania kutopuuzia utabili wa wake kwani ni hakika damu itamwagika kama watu wataavutana kama nilivyoona katika mabasi yale.

Dr Mwasumbi, aliwahi kupata maono mwaka 1996 kuwa mvua kubwa ya elimino ingeweza kunyesha hapa nchini Tanzania, utabiri wake ukaja kutimia mwaka 1998 ambapo mvua kubwa ya kutisha ilinyesha.

Mbali na hilo pia alitabiri ujio wa Rais John Pombe Magufuli, rais ambaye anachukia rushwa, hatapanyi fedha, alipata maono juu ya utajili mkubwa katika taifa, kutokana na hilo Mungu alimwambia nabii habari ya kuja kiongozi mwenye uchungu nan chi hii, na mtendaji mzuri, hapo ndipo mashamba ya Tanzania yatakapoanza kutoa mali za thamani kama vile mafuta, madini vitu ambavyo vilikuja kutokea.

Ends,


Maoni 3

Amulike alisema ...

Mungu atusaidie kwakweli

Sarah alisema ...

Mungu wa Mbinguni aendelee kuipigania nchi ya Tanzania
Barikiwa mtumishi

Unknown alisema ...

Hakika tunazidi kumwona Mungu wa Nabii Kennedy Mwasumbi kwa namna ya pekee sana hakika huyu ni nabii wa Mungu