Kuwaficha wanaofanya rushwa ya ngono ni kuchochea ubakaji-WAJIKI
Na Selelmani Magali
Asasi ya wanawake katika jitihada za maendeleo (WAJIKI) imesema wadau mbalimbali wakiwamo madereva wa bodaboda, wazazi na madereva wa magari wanapaswa kuunganisha nguvu kupinga vitendo vya ukatili wa kingono kwani ukiendelea kuachwa ulivyo unaweza ukachochea ubakaji.
Akizungumza na madereva wa bodaboda katika viwanja vya relini, Gongo la Mboto, Wilaya ya Ilala jijini Dar es salaama, Mkurugenzi wa Asasi ya WAJIKI, Janeth Mawinza alisema tatizo la ukatili wa kingono bado ni kubwa na linahitaji nguvu ya pamoja ili kulitokomeza.
UMBALI mrefu, changamoto ya usafiri ni mojawapo ya mambo yanayoelezwa kuchangia kuendeleza ukatili wa kingono kwa wanawake na wanafunzi nchini.
Usafiri unatajwa kuwa mbinu rahisi kwa madereva wa bodaboda na magari wakiwamo utingo kutumia kama mtego wa kuwanasa watoto wa shule za msingi na sekondari ambao husafiri umbali mrefu kuisaka elimu.
Akizungumza katika kampeni ya kupinga ukatili wa kijinsia nchini iliyoandaliwa WAJIKI kwa ufadhili wa Women Fund Tanzania, Mawinza alisema wanawake na wanafunzi wamekuwa waathirika wakubwa kutokana na shida ya usafiri katika mkoa wa Dar es Salaam
“Mimi naendesha bodaboda hapaGongo la Mboto nashuhudia mengi kwa madereva, wanatumia changamoto ya usafiri kufanya ngono kirahisi, mwanamke anajikuta hawezi kukataa kwa sababu ana shida,” alisema Msafiri Adam.
Kauli ya Adam imekuja ikiwa serikali tayari imetangaza kuandaa mpango wa taifa wa kutokomeza ukatili wa kijnsia dhidi ya Wanawake na Watoto kwa asilimia 50 ifikapo mwaka 2022.
Mpango huo ni sehemu ya utekelezaji wa Sera ya Maendeleo ya Wanawake na Jinsia (2000); Mkakati wa Taifa wa Maendeleo ya Jinsia (2005); Sera ya Maendeleo ya Mtoto (2008); Sheria ya Makosa ya Kujamiiana – SOSPA (1998).
Madereva ni wadau wakubwa hivyo wanawajibu wa kuwalinda wanawake na watoto, wavunje ukimya na kutoa taarifa na kukemea vitendo vya ngono.
Janeth Mawinza alisema kuna mambo mengi yanayochangia muendelezo wa ukatili wa kingono kwa watoto wa shule lakini umbali nao umechangia kuendelea kuwapo kwa ushawishi wa kushiriki ngono kwa baadhi ya wasichana na mwishowe kupata mimba.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni