Dulla Mbabe, Twaha Kiduku kuzipiga Agost 28,2020
Na Mwandishi wetu,
Ule mpambano uliokuwa
unasubiliwa kwa hamu kati ya bondia Dulla Mbabe na Mpinzani wake Twaha Kiduku
hatimaye taratibu zake zimekamilika na unatarajiwa kuchezwa Agost 28, 2020
katika uwanja wa uhuru.
Itakumbukwa kuwa kwenye
pambano la kwanza kati ya Dulla Mbabe na Twaha Kiduku upinzani ulikuwa mkubwa
sana na wengi wanaamini Twaha ndiye aliyeshinda pambano lile japo maamuzi ya
majaji yaliamua sare.
Kuondoa utata huo,
Promota J msangi ameleta pambano hilo sebuleni kwako, ni mpambano ambao hupaswi
kuukosa, ni mpambano wa kumaliza ubishi.
“Siku ya tarehe
28/8/2020 tutashuhudia tena kwa mara ya pili mpambano wa kukata na shoka kati
ya bondia Dulla Mbabe na mpinzani wake Twaha Kiduku, wakazi wa Dar es salaam na
mikoa ya jirani mjitokeze kushuhudia mpambano huu, itakuwa burudani ya aina
yake,” alisema Promota Mssangi.
Ubishi wa nani
alishinda pambano la kwanza Sasa utaenda kumalizwa tarehe 28/8 hapo uwanja wa
uhuru jijini dar es salaaam. Twaha mara kwa mara amekuwa akilalamika kwamba
Dulla amekuwa akimkimbia mara kwa mara kwa kuhofia kupokea kipigo kitakatifu
kutoka kwake.
Akizungumza na
fullhabari blog, Twaha Kiduku, kijana anayefanya mazoezi chini ya milima ya
Ulugulu, ameahidi kurudisha heshima mkoani Morogoro.
“Dulla fanya
mazoezi vinginevyo…. Shoo…shoo…shoo..haipingi nitampiga au anipige lakini
raundi 12 haziwezi kuisha, mtu mmoja lazima alambe sakafu,” alijinasibu Twaha
Kiduku.
Kwa upande wake
Bondia Dulla Mbabe naye alitoa kali yam waka baada ya kuahidi kukwata pesa zake
katika mkataba wakae aliosaini kucheza pambano hilo ili alipwe Bondia Twaha
Kiduku.
Alisema yeye kwa
hiari yake ameamua kuruhusu jumla ya Shs. 200,000 kukatwa kutoka fedha yake
iliyo kwenye mkataba na amesaini makubaliano hayo kimaandishi mbele ya promota
Msangi kuonyesha kuwa hatanii katika dhamira yake hiyo.
Katika mahojiano
maalum, Mbabe alisema yeye ni bondia asiyepigika, Nchini China hawamtaki kwa
kuwapiga mabondia wao kipigo kitakatifu, lakini pia Twaha sio bondia bali ni
bausa atampiga ili arudi akamlinde Babu Tale kwenye ubunge wake huko Morogoro
kusini mashariki.
Mpambano huo
unavuta hisia kwa watu tofauti, unatarajiwa kuvuta watu wengi sana.
Sasa mbivu na
mbichi zitajulikana siku hiyo , ngoja tuendelee kusubiri.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni