WANAWAKE WATAKA KUUZA ALIZETI YAO KAMA BIDHAA BADALA YA MALIGHAFI
Vikundi
vya wanawake vya Tumaini Group na Mkombozi Group vilivyopo kata ya
Sakasaka wilayani Meatu mkoani Simiyu wamesema hawatauza tena alizeti
kama malighafi bali watauza kama bidhaa kutokana na tathmini walizoziona
kwenye zao hilo.
Hayo
waliyabainisha wakati wanapoendelea na maandalizi maonesho ya Nane
Nane yanayotarajia kufanyika kwa mwaka wa tatu sasa kama ilivyo agizo la
serikali katika mkoa wa Simiyu ifikapo Agosti 8 mwaka huu.
Walidai kuwa kuuza malighafi kumewachelewesha kufikia malengo ya kundi
hilo pamoja na maendeleo ya mtu mmoja mmoja kwani wamekuwa wakipata pesa
kidogo ukilinganisha na mafuta ya zao hilo.
“Tumekusudia tuuze alizeti zetu baada ya kuchakata mafuta na kwa gunia
moja linatoa lita 17 za mafuta na ukiuza unapata shilingi 60,000/= au
55,000/=/= na ukiuza alizeti bila kusindika unapata 30,000/= ambayo ni
hasara kwa mkulima na kikundi, kwa gunia zetu 12 kikundi kitapata faida
kubwa itatusaidia kusomesha watoto na maandalizi ya mashamba kwa
mwakani” alisema Bi. Christina mhasibu wa Mkombozi Group
“Mradi huu wa alizeti tuliofadhiliwa na REDESO umetupatia manufaa kwani
mwaka jana tulipouza mafuta ya alizeti pesa zile zilitusaidia
wanakikundi kwani tulikopeshana kwa lengo la kuanzisha miradi ya mtu
binafsi wakati tusipokuwa na alzeti tukakopeshana pesa kila mtu 50,000
kwa liba ya 10% wapo waliolima pamba,karanga na hata mahindi pia na
vinatusaidia”,alisema Mwenyekiti kikundi cha Tumani Bi.Elizabeth Bisha.
Mbali na hayo, Afisa maendeleo ya jamii kata ya Sakasaka wilayani Meatu
mkoani Simiyu Bi. Mbuke Jaulula aliwataka akina mama wakulima wa
vikundi vilivyoko katika kata hiyo kuendelea kuwapa wanawake na
wanajamii wengine elimu juu ya ulimaji wa zao la alizeti licha ya kuwa
linasitahimili ukame bali pia ni zao lenye faida kwa kutoa mafuta na
hata chakula cha mifugo lakini pia kwa mwezeshaji wa kikundi hicho
ambaye ni REDESO apate mrejesho mzuri dhidi ya matarajio yao
wanayoyategemea baada ya kuwawezesha wanakikundi.
“Mwaka huu tumewezeshwa na REDESO mbegu bora za alizeti kwa vikunndi
vinne na tumevuna gunia 2 hadi 3 kwa hekali kwa magunia ya debe 6 na
tutanufahika pakubwa hivyo niwasihi wanajamii wa kata ya sakasaka hasa
wanawake wa jamii hii ya kisukuma kwa kuwa bado kuna mila kandamizi,
kupitia kilimo hiki tuwe na amasa zaidi ya ufugaji wa kisasa
ikilinganishwa na kuwa tunaishi pembezoni mwa hifadhi na kukosa sehemu
ya malisho kwa kulima zao hili tutapata chakula cha mifugo pia na
hawatahangaika”aliongeza Bi. Jaulula.
Kwa upande wake Mratibu miradi na Meneja kutokea asasi isiyokuwa ya
kiserikali REDESO inayofanya kazi wilayani Kishapu mkoani Shinyanga na
baadhi ya kata za wilaya ya Meatu mkoani Simiyu Bw. Charles Buregeya
amewapongeza wanakikundi hao huku akiwataka wasiridhike kwa mavuno hayo
bali waendeleze bidii na jitihada katika uzalishaji ili waweze kufikia
angalau gunia 7 hadi 8 kwa hekali moja kama inavyoshauliwa kitaalamu.
“Lakini pia kijasiriamali mmeonesha ukomavu kwani kuuza alizeti peke
yake hautapata tija ukilinganisha na mafuta ila ninachotaka mkizingatie
ni kuhakikisha mmeboresha uzalishaji,usindikaji na vifungashio ili
tuweze kuingia kwenye ushindani na pia tuhakikishe tunatafuta masoko ili
tuweze kuingia kwenye soko la ushindani, na pia shukrani kwa serikali
kupitia maendeleo ya jamii kwa ushirikiano wanaotupatia”,alisema
Buregeya.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni