Veta Kihonda wataka madereva wajiendeleze kielimu
Mwalimu wa magari ya mizigo kutoka Veta
Kihonda, Willium Munuo akifafanua jambo kwa waandishi wa habari katika viwanja vya sabasaba.
Kufuatia kuimalika kwa sekta ya usafirishaji, kuongezeka kwa barabara za juu, wito umetolewa kwa madereva hapa nchini kuangalia umuhimu wa kujiendeleza kielimu ili waweze kuwa Bora katika kazi zao.
Akizungumza katika maonyesho ya sabasaba, mwalimu wa magari ya mizigo kutoka Veta Kihonda, Willium Munuo alisema Kuna haja ya madereva kwenda kusoma.
Alisema mbali na teknolojia ya magari kubadilika kila Leo lakini pia miundo mbinu ya barabara nayo imekuwa ikiimarika kila kukicha.
"We angalia mfumo wa ubungo interchange, pale madereva wasipokuwa na weledi watagongwa Sana, ndio maana nasema waje kwetu wasome, waongeze uelewa wao" alisema
Kuhusu mafanikio ambavyo wameyapata kwa mwaka huu, Mwalim Munuo alisema wameweza kufunza zaidi ya madereva 1700, Jambo ambalo wanaamini uwepo wa madereva hao sokoni utapunguza ajali za barabarani
"Lengo letu sisi ni kupunguza ajali za barabarani, hivi Sasa idadi ya wataalamu wa udereva inaongezeka, hilo limepelekea kupungua kwa makosa madogomadogo barabarani, pia hata tochi nazo zimepungua, hakuna kesi nyingi za mwendo kasi Kama zamani, alisema Munuo
Maoni 1
Na Mimi nlikuwa naomba kusomea udereva wa magari makubwa
Chapisha Maoni