Watakao andamana sabasaba nyeupe kukiona
Jeshi la Polisi kanda Maalum Dar es salaam limetoa onyo kwa kikundi au
mtu yeyote atakayeshiriki maandamano Siku ya 77 kesho Julai 7, 2020.
Kamanda Lazaro Mambosasa ametoa onyo hilo leo alipozungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam, na kubainisha watakaofanya maandamano hayo batili watashughulikiwa kwamujibu wa sheria.
“Jeshi linatoa onyo kali kwa kikundi au mtu yeyote, atakaye shiriki maandamano hayo batili, kwa madai ya kudai tume huru ya uchaguzi, waache mara moja vinginevyo watashughulikiwa kwamujibu wa sheria” Ameonya Mambosasa.
Maandamano hayo yalianza kuhamasishwa kwenye mitandao ya kijamii kwa madai ya kudai Tume huru ya Uchaguzi kwa kutumia hashtag ya 77 nyeupe.
Wazo la kuyafanya kwaajili ya kudai tume huru ya uchaguzi liliibuliwa hivi karibuni na Dkt. Benson Bagonza ambaye ni askofu wa kanisa la Kilutheri Tanzania, Dayosisi ya Karagwe mkoani Kagera.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni