Veta Pwani yabuni meza yeneye uwezo wa kupasha joto chakula
Mwalimu wa Chuo cha Ufundi stadi Veta Pwani Haji Sinani anayefundisha kozi ya majokofu na viyoyozi, akizungumza na Mwandishi wa habari hizi.
Chuo cha Ufundi stadi Veta Pwani imebuni
meza ya aina yake ambayo inauwezo wa kupasha joto chakula na kuweka
baridi katika vinywaji inayoweza kutumiwa sehemu yoyote.
Akizungumzia
na FULLHABARI BLOG, katika viwanja vya maonesho sabasaba, Mwalimu wa Chuo
cha Ufundi stadi Veta Pwani Haji Sinani anayefundisha kozi ya majokofu
na viyoyozi amesema meza hiyo imebuniwa ili kuondoa adha ya vinywaji
kupoa.
Sasa Wamiliki wa migahawa na hoteli huenda
sasa wataondokana na ile shida ya baadhi ya vyakula vya wateja kupoa
kikiwa mezani au kuganda.
Mbali na kuganda pia
huenda wamiliki hao wakavutia wateja wao zaidi kutokana na vinywaji vyao
kuendelea kuwa baridi hata kama atakunywa kwa saa zima.
Sinani
wazo la kuja na meza hiyo lilitokana na kuona adha wanayopitia watoa
huduma ya chakula kulazimika kutumia ‘oven’ katika kupasha chakula
kilicho ganda wakati mteja akiendelea kula.
“Hii
itawarahisishia wamiliki was mahoteli kufanya mambo yao kwa ufanisi na
kuvutia wateja wengi katika shughuli zao wanazofanya,” alisema Sinani
Alisema
meza hiyo imefungwa injini ya jokofu chini na kutengenezewa mfumo wa
baridi katika matundu maalumu ya kuweka chupa za vinywaji au glasi ili
kuweza kuendelea kupoza vinywaji vyao.
Alisema
katika utengenezaji wa meza hizo huzingatia zaidi mahitaji ya wateja
hivyo huweza kuwa na matundu manne ya kupozea vinywaji na sehemu moja ya
kuchemshia chakula au kuongezwa idadi.
“Unaweza
kuweka matundu nane ya kupozea vinywaji na matundu mawili ya kuchemshia
chakula ni wewe tu kulingana na mahitaji yako na inatumia umeme kama
kawaida,” alisema Sinani
Alisema meza hizo huweza
kutumia injini moja ya jokofu au ya zamani kulingana na mahitaji ya
mteja huku meza hizo zikiwa tayari kwa ajili ya kuuzika
Hakuna maoni
Chapisha Maoni