Nimeisambaratisha CHADEMA Ukonga, sasa nahamia Tarime Vijijini- Mwita Waitara
Naibu
Waziri wa TAMISEMI Mwita Waitara, amesema kuwa mpaka sasa hivi
amekwishamaliza kazi kubwa ndani ya Jiji la Dar es Salaam ya
kukisambaratisha Chama cha CHADEMA, na kwa sasa ameweka wazi kwa mara
nyingine kuwa atakwenda kugombea ubunge katika jimbo la Tarime Vijijini
mkoani Mara kupitia chama hicho.
Waitara
amesisitiza kuwa haondoki Ukonga kwa sababu anamkimbia mtu, bali
amekamilisha kazi ya kukisambaratisha Chama cha Demokrasia na Maendeleo
(CHADEMA), hivyo anakwenda Tarime Vijijini ambako ndipo anapotokea,
kufanya kazi hiyo.
“Wala
hakuna mtu ninayemkimbia, jimbo langu [Ukonga] lipo salama ndani na nje
ya chama. Nimeshafanya kazi ya kuwasambaratisha CHADEMA hapa
wameshapoteana. Walikuwa na Meya wa Jiji, hayupo, walikuwa na Meya
Ilala, hayupo, walikuwa na Meya wa Ubungo, hayupo. Nishamaliza kazi Dar
es Salaam, naenda kukamilisha kazi sehemu nyingine,” amesema Waitara.
Kiongozi
huyo ambaye alihamia CCM akitokea CHADEMA Julai 2018 amesema kuwa Julai
14 mwaka huu atachukua fomu ya kuomba kuteuliwa kugombea ubunge Jimbo
la Tarime Vijijini, na kwamba suala hilo sio siri.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni