Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta Alegeza Masharti Ya Kukabiliana Na Corona
Rais
wa Kenya Uhuru Kenyatta amelegeza kwa kiasi fulani sheria kali
zilizokuwa zimewekwa kwa ajili ya kukabiliana na maambukizi ya ugonjwa
wa COVID-19
Akilihutubia
taifa hilo leo Jumatatu katika Jumba la Harambee jijini Nairobi, Rais
Kenyatta ametangaza kuondoa marufuku ya safari ya watu kuingia au kutoka
katika kaunti za Nairobi, Mombasa na Mandera kuanzia kesho Jumanne.
Hata
hivyo amesema kuwa agizo la kutotoka nje kuanzia saa tatu usiku hadi
saa kumi alfajiri litaendelea kuwepo kwa kipindi cha siku 30 zijazo.
Vile
vile, Rais Uhuru Kenyatta amesema makanisa na misikiti itafunguliwa
lakini waumini wasiozidi 100 ndio watakaoruhusiwa kuhudhuria ibada na
kwa muda usiozidi saa moja. Shule za Jumapili na madrasa zitasalia
kufungwa kwa muda wa siku 30.
Hali
kadhalika Rais wa Kenya amesema safari za ndege za ndani ya nchini
zitaanza Julai 15, huku zile za kimataifa zikitazamiwa kuanza Agosti
Mosi, lakini kwa kufuata tahadhari za kiafya.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni